Tuesday, September 8, 2015

SHIRIKISHO LA VYUO VIKUU TANZANIA LAMUUNGA MKONO MH. JOHN MAGUFULI


Hatimaye shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania wametangaza nia yao ya kumuunga mkono Dr John Pombe Magufuli kutokana na sera zake mahususi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu. Aidha wanafunzi hao wa vyuo vikuu kwa nyakati tofauti wamesema kumekuwa na changamoto ya mikopo iliyokuwa ikiwakabili kwa muda mrefu,hivo ujio wa DR Magufuli sasa changamoto hiyo ni basi.

Dr Magufuli ameonyesha njia thabiti za kuhakikisha kila mwanafunzi anapata stahiki zake kwa wakati na bila usumbufu. Aidha ktka mikutano yake Dr AMEKUWA AKISISITIZA wanafunzi hao wanapaswa kusoma kwa bidii na baadaye kuja kulitumikia Taifa,Serikali itatengeneza miundo mbinu thabiti, viwanda kwa ajili ya wahitimu mbalimbali kupata ajira mara baada ya masomo yao.

Kutokana na hali hiyo wanafunzi wote wa vyuo vikuu nchini wamefurahishwa sana na namna Dr Magufuli atakavyomaliza adha hiyo iliyokuwa ikiwakabili, hivo wamesisitiza kuwa nae ktka kumuongezea ushindi wa KISHINDO.

Wanafunzi hao pia wamesisitiza kutoa ushawishi kwa makundi mengine ktk jamii na hata ngazi ya familia, kutoa elimu kwa makundi hayo juu ya utekelezaji wa agenda hizo ili Dr Magufuli aweke historia ya Dunia kwa kupata ushindi wa kishindo.

Aidha wameitaka tume ya uchaguzi kuwa makini na itakapobidi kuchukua hatua stahiki kwa wagombea wote wanaotanguliza udini na ukanda ktka kampeni zao

HONGERENI SANA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KWA JUHUDI ZENU KTKA KUONGEZA USHINDI KWA DR JOHN POMBE MAGUFULI

No comments:

Post a Comment