Kongamano hilo liliandaliwa na Wanawake Vyuo Vikuu wakishirikiana na Wanawake Wasomi na Wanawake Vyuo Vikuu. Ukumbi wa Diamond Jubilee ulifurika wanawake zaidi ya elfu tatu.
Ni kwa mara ya kwanza katika historia ya wanawake vyuo vikuu kuweza kukutanisha wanawake vyuo vya elimu ya juu zaidi ya 18 Dar wa salaam kwa mara moja.
Aidha kongamano lilihudhuriwa na wanawake mbalimbali kutoka Serikalini, vyama vya upinzani, dini nk
Mada kuu"MWANAMKE AMEWEZA APEWE FURSA ZAIDI"
Mada zilizojadiliwa ni:-
1. Vipaumbele Vya Mwanamke
2. Huduma za Jamii
3. Mwanamke na Umilikaji wa Rasilimali
4. Mwanamke na Uchumi
Professor Bertha Koda na Prof Martha Oorro waliongoza maelfu ya wanawake vyuo vikuu.
Mgeni Rasmi alitambua nafasi ya mwanamke mwenzie kutoka ACT WAZALENDO ambaye hakuwepo kutokana na ratiba ya kampeni.
Wanawake walitoa pongezi nyingi kwa chama cha CCM na ACT WAZALENDO kwa kutambua nafasi ya mwanamke kwa vitendo na kuteua wanawake kwenye nafasi ya Urais na Makamu wa Rais. Vyama vingine vinapiga porojo kumheshimu mwanamke lakini nafasi hapewi, wanamtumia mwanamke Kama mtaji wa kuombea kura. Hongera sana CCM, nyie ni watu wa vitendo na sio maneno.
Aidha wanawake hao waliipongeza CCM kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya wanawake kwenye nafasi za Ubunge na Udiwani kuliko chama kimgine chochote. Wanawake tumefarijika sana sana na kura zetu mtapata.
Kwa msisitizo wanawake wanadai 50 kwa 50. Angalau CCM imeonesha kulijali hilo hivyo kupata kura nyingi za wanawake.
Aidha Mgeni rasmi alieleza vizuri namna atakavyosimamia mazingira, kuratibisha biashara za wanawake na vijana, kusimamia kikamilifu huduma za jamii, kutoa mikopo yenye RIBA nafuu kwa wafanyabiashara ndogo ndogo, kutoa bima ya Afya kwa watu wote nk
Naomba kuwasilisha.
No comments:
Post a Comment