Saturday, September 26, 2015

Hussen Bashe, Mwigulu Nchemba na Emmanuel Nchimbi waisimamisha Nzega


Hussein Bashe akiaongea na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni Aliyekuwa rafiki mkubwa wa LOWASSA wakati akiwa ccm Bw Hussein Bashe amezindua kampeni zake za ubunge kwa mafanikio makubwa Katika jimbo la Nzega mjini ambapo umati mkubwa wa watu umeudhuria uzinduzi huo wa kampeni hiyo kwa siku ya jana .

Ikumbukwe Bw Bashe Alikuwa ni kiungo muhimu sana wakati Lowassa akisaka Urais kupitia CCM lakini baada ya Lowassa kuhamia Chadema Bw Bashe ameendelea kubaki ccm na ndiye mgombea wa ubunge katika jimbo la Nzega mjini kwa tiketi ya CCM,

Wachambuzi wa siasa katoka jimbo hilo wanasema uwezekano wa Bashe kushinda ubunge katika jimbo hilo ni mkubwa kutokana na yeye kujijenga kwa muda mrefu kwasababu amekuwa yupo karibu na wanachi hasa kwa upande wa kutoa misaasda kwa makundi muhimu mfano vijana ,wanawake,

CHINI ni kauli ya Hussein Bashe kupitia ukurasa wake wa facebook
LEO HII KATIKA UZINDUZI WA JIMBO LA NZEGA MJINI!!NACHOWEZA KUSEMA NI;
ASANTE WANA NZEGA,
ASANTE COMRED NCHIMBI NA MWIGULU NCHEMBA.

Hussein Bashe katikati akiwa na makada wa ccm wakati wa uzinduzi wa kampeni za ubunge
Hussein Bashe akiongea na wananchi wakati wa mkutano

No comments:

Post a Comment