LOWASSA ASEMA UONGO KUHUSU MTAMA YA NAPE NA CCM
NI AIBU watu wazima kusema Uongo; MTAMA ya NAPE na CCM.
Nimeshitushwa na taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari ambazo zimedai wanachama 16,746 wa CCM kitongoji cha Mtama wamerudisha kadi za Chama hicho na kujiunga na CHADEMA...nilistuka sana.
Kwa mara ya kwanza nilipoiona habari hiyo hapa JF nikajua ni muendelezo wa #ULOFA ambao nimeuzoea hapa jukwaani, lakini nilipousikia na kuuona kwenye TELEVISHENI nikaona sio jambo la kupuuzwa tena, ni lazima liwekwe sawa.
Taarifa hiyo ni ya UONGO uliokubuhu, na ufuatao ni UKWELI HALISI kuhusu wanachama wa CCM jimbo la Mtama, nitaandika kwa mukhtasari.
Jimbo zima la Mtama lina wanachama wa CCM "waliohakikiwa" = 16,762 kati yao Mabalozi takriban 3,000, Viongozi wa Wilaya, Kata, Matawi na Mashina. Ni vichekesho kusema kuwa kati ya wanachama 16,762 wanachama 16,742 wamehama na hivyo CCM ina wanachama 16,762 - 16,742 = 20 Ni vichekesho.
Sensa ya watu na Makazi, imetaja WAKAZI wa Kitongoji cha Mtama ni 4,398 ambapo wanaume ni 2,029 na wanawake 2,369. Ni MIUJIZA ya wazi kuweza kupata wahudhuriaji zaidi ya 20,000 katika sehemu yenye wakazi 4, 398 na ikimbukwe idadi hiyo ni pamoja na watoto wachanga na vikongwe...yaani ikiwa hakuna mtu ambaye anabaki NYUMBANI basi tulitegemea mkutano wa LOWASSA uwe na wahudhuriaji 4,398..lakini sinema na maigizo kuwa wamepata watu zaidi ya 20,000 na 16,742 wamerudisha kadi ni VICHEKESHO..
MTU MZIMA ANAPOAMUA KUONGEA UONGO TENA HADHARANI, UJUE AMESHAZIDIWA NA MAJI YAMESHAFIKA SHINGONI...Lakini kwa kuwa UONGO daima haudumu mwisho wa siku wanadhalilika kama hivi...
No comments:
Post a Comment