Tuesday, September 15, 2015

TAARIFA YA MAANDAMANO LEO KUANZIA SAA NANE MCHANA-MOROGORO MJINI SASA ZAMU YETU

Kutakuwa na maandamano makubwa ya Wanachama wa Chadema, kuunga mkono msimamo wa aliyekuwa Katibu Mkuu wetu Dr. Wilbroad Slaa kupinga Mapinduzi ya misingi ndani ya Chadema, kwa kumkaribisha fisadi kutoka CCM kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya chama chetu. Vile vile tunapinga kitendo cha uongozi wa Chadema Taifa kumdhalilisha na kumtukana Dr. Slaa kwenye vyombo vya habari huku wakisahau mchango wake mkubwa katika kujenga Chadema. Tunapinga kitendo cha Chadema kumpokea Fredrick Sumaye ambaye kashfa zake za Ufisadi na kukandamiza upinzani zinafahamika. Tunaandamana kutaka maelekezo kwamba kama tumewafukuza Said Arfi, na Zitto Kabwe kwa tuhuma za usaliti, tunawezaje kuwapokea watu ambao walikuwa makada wa CCM kwa zaidi ya miaka 30? Tunaandamana kupinga kitendo cha Chadema kuwapokea watu kama Makongoro Mahanga ambaye alituibia kura mwaka 2010 jimbo la Segerea, na Lawrance Masha ambaye alishiriki kukandamiza harakati zetu jimbo la Nyamagana.


Tunawakaribisha Watanzania wazalendo kutoka CUF na NCCR kupinga ubakaji huo wa demokrasia uliofanywa na Freeman Mbowe.



Tunaandamana kuishinikiza serikali wamnyang'anye sumaye mashamba yetu morogoro
Maandamano yataanzia katika nane hadi msamvu.



Anthony Temu, 


Mratibu wa Maandamano
0754226498

No comments:

Post a Comment