Wednesday, September 16, 2015

MREMA WA 1995 ALIKUWA NA NGUVU SANA KULIKO LOWASSA WA 2015

Mrema ndiye mpinzani pekee aliyeitetemesha hasa CCM kuliko mtu yeyote mpaka sasa.

1. Mrema alikuwa anapambana na Mkapa ambaye wengi hawakumjua.. Tofauti na sasa Lowassa anashindana na Jembe Magufuli a.k.a. JEMBE linalo Julikana.
2. Mrema alikuwa one Man army. Aliondoka CCM pekeyake bila kuwa na Msafara kama Lowassa na bado alitisha sana.
3. Mrema hakuwa na ma twitter, WhatsApp, Fb, Jf, Radio wala Wahariri wa Magazeti wanao mpamba pamba kila siku kama Lowassa na bado alitisha.
4. Mrema alikuwa hot cake kweli, wakina mama walilia, watu walizimia, vijana waliweweseka kila walipo mwona.
5. Ni Mwl. Nyerere na Mrema tu ambao walitandikiwa kanga wapite mara nyingi zaidi.
6. Mrema alipendwa hasa, alipo ondoka CCM vyama vyote vya SIASA vilimtaka, Wenyeviti hawakulala... Kila siku kwa Mrema kumbembeleza ahamie kwao.
7. Mrema alipendwa haswa, watoto wengi waliozaliwa 1995 waliitwa Augustino, kwa kumuenzi shujaa wao.
8. Mrema alikuwa ni biashara hasa, chochote kilichowekwa picha ya Mrema kilinunuliwa kwa bei yeyote ile.
9. Mrema hakuhitaji mapesa ya Kujisafisha wala hakuwa na matajiri weeengi wakumsapoti kama Lowassa, aliishi kwa harambee na michango ya watanzania lakini bado alitisha.
10. Mrema wa 1995 alikuwa na rekodi nzuri sana ya uchapakazi kuliko Lowassa wa 2015 ambaye amezuungukwa na kashfa Lukuki za upigaji DILI. Kwa maneno mengine Lowassa ni brand iliyotengenezwa kwa pesa kwa ufanisi mkubwa na maigizo ya kutosha lakini Mrema ilikuwa ni nguvu hasa ya wananchi.
11. Mrema alipambana na CCM na waasisi wa CCM akiwemo Mwl. Nyerere na bado alitisha sanaaa tofauti na Lowassa anapambana kipindi ambacho waasisi kama Nyerere na Kawawa hawapo, na ambao walikuwa na nguvu sana.


Pamoja na yote CCM ilishinda 1995 na itashinda kwa kishindo 2015.

No comments:

Post a Comment