Wednesday, September 16, 2015

DARAJA LA KIKWETE, ALILOZINDUA RAIS KIKWETE JANA



Mdau mkubwa wa Globu ya Jamii mjini Dodoma Bw. Gama akifurahia kukamilika na hatimaye kuzinduliwa kwa Daraja la Kikwete juu ya mto Malagarasi mkoani Kigoma. Anasema Mnyonge Mnyongeni, haki yake mpeni. Jk ameifanyia makubwa nchi ya Tanzania katika utawala wake wa awamu ya nne hata kama wapinzani watajifanya vipofu na kutoona maendeleo haya aliyoleta JK na ambayo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli amepania kuchukua baton na kuendeleza kwa kasi kubwa mbio za Maendeleo na Maisha bora kwa kila mtu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Kikwete akipeana mikono na Balozi wa Korea Kusini Mhe. Chung II, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Luteni Kanali Mstaafu Issa Machibya na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga mara baada ya ufunguzi wa Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Jakaya Kikwete akiwa pamoja na mkewe Mama Salma Kikwete katika picha ya pamoja na ujumbe wa Korea Kusini uliojenga Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi mara baada ya kulifungua rasmi Daraja hilo lenye urefu wa mita 275 na barabara unganishi zenye urefu wa Km. 48.
Muonekano wa Daraja la Kikwete katika Mto Malagarasi lenye uwezo wa kubeba tani 180 na kudumu kwa miaka 100 kama likilindwa na kupitisha mizigo isiyozidi uzito.

No comments:

Post a Comment