Wednesday, September 16, 2015

DARAJA LA KIGAMBONI NI LA KWANZA KWA UKUBWA AFRIKA MASHARIKI

Kumwaga sumu ni kwa faida ya nani?

Napata shida sana kuelewana na mtu anayesema:

1. CCM haijafanya kitu kwa miaka 50.

2. Barabara, madaraja, shule, na miradi mingine ya maendeleo haijajengwa kwa fedha za CCM.

Kwa kauli ya kwanza ina maana Tanzania ya mwaka 1961 na Tanzania ya leo ziko sawasawa? Hakuna kilichoboreshwa?

Au Tanzania ya toka ulipoanza darasa la kwanza na ya leo ziko sawasawa? Hakuna kilichoboreshwa?

Na kwa kauli ya pili inabidi tu niwaulizage (a) Je unajua maana ya serikali? na (b) Je CHADEMA inaomba kupewa madaraka ili ijenge nchi kwa pesa za Ndesamburo na Mtei na Billicanas?

Fanyeni kampeni zenye weledi. Watanzania wengi sio wachambuzi wa mambo ila msiwadanganye kwa hoja za kumwaga sumu. Sumu itaangamiza taifa, sio CCM tu.


No comments:

Post a Comment