Aliyejiuzuru Uwaziri Mkuu kwa kashfa za Richmond alizotuhumiwa bungeni Edward Lowassa, ambaye pia ni Mgombea wa Kiti cha Urais kupitia Ukawa hana Sera.
Kimsingi Lowassa ana jina kubwa lakini hana sifa au sera anazoeleza wazi nini atakachofanya akiwa Rais kama ilivyo kwa Mh. John Magufuli mgombea wa kiti cha Urais kupitia CCM na wagombea wengine kama wa ACT Wazalendo. Sera tunazozisikia ni kutoka Mh. John Magufuli zenye mshiko na upeo wa hali ya juu sana. Kwa upande wa Lowassa, yeye amebakia kusema pipozz kama vile hiyo ndio sera yake pekee, zaidi ya hapo, Lowassa anawarubuni watu kwa kusema atatoa elimu Bure huku Mgombea wa CCM Mh John Magufuli anasema yeye atatoa elimu BORA.
Lowassa hana sera ni kujipitishapitisha na kuhudhuria mikusanyiko ya kutengeneza ya UKAWA iliyo jaa chuki na isiyo na Sera.
Tanzania ya leo si ile ya kuchagua umaarufu wa mtu au umaarufu wa kujulikana, tunahitaji Sera.
Tanzania ya leo hatuhitaji kujionyesha kwa kupitapita kila sehemu kwa kusema Pipozzz, tunahitaji uuzaji wa sera utaibadilishaje Tanzania ya leo tuwe na Tanzania tuioteayo. Mh. Magufuli anaendelea kumwaga sera zake kila mkoa na jinsi gani ataibalisha hiyo mikoa.
Lowassa, tunataka utuonyeshe kwa nini hukuweza kushughulikia matatizo ulipokuwa Waziri Mkuu, Mbunge kamati ya bunge na uongozi katika ngazi mbalimbali chamani.
Kama hayo hukuweza kuyashughulikiwa upolikuwa Waziri Mkuu, Waziri, Mbunge, mwenyekiti kamati ya bunge, ngazi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama na kuhitimishwa kwa kashfa ya Richmond hadi ukajiuzuru, utawezaji kurejesha imani kwa wananchi na kuondoa uchafu unaoendelea ndani ya serikal hasa ubadhilifu wa mali ya umma na Ufisadi?
Lowassa hana SERA.
Mr. Chin
No comments:
Post a Comment