Tuesday, September 1, 2015

DR. SLAA AKIZUNGUMZA NA MEDIA SERENA HOTEL: SOMA "TRANSCRIPTS" ALIYOYASEMA KUHUSU LOWASA


Name:  Slaaa.png
Views: 3162
Size:  316.4 KB


Slaa: Watanzania wana kiu ya kujua kwanini amekuwa kimya kwa muda mrefu sasa licha ya harakati za kisiasa kuendelea. 


Muda utakaotumika ni saa moja, hakuna muda mrefu sana.

Ameamua kufanya hayo kwa kuwa imefika mahali ukweli lazima usemwe na upotoshwaji ukomeshwa. Namna pekee ya kufanya hivyo ni kutoka hadharani na kuusema ukweli.

Sote tunafahamu kuwa hana tabia ya kuchenga mambo, mengi yamesemwa na watu tofauti, kwenye mitandao, magazeti na viongozi wake!

Hana ugomvi na kiongozi yoyote, kwa kuwa siasa sio ugomvi. Kama binadamu wa kawaida hana chuki wala hasira na binadamu mwingine yoyote!

Iwe wazi kuwa katika Taifa kuna misingi ambayo inaongoza taifa. Inapofika mahali taifa linaongozwa kwa msingi ya propaganda na upotoshwaji matokeo yake ni vurugu kubwa katika taifa. Yeye amekataa hayo yote!

Anasema kuwa YEYE hakuwa likizo kama inavyosemwa na viongozi wake! Atafafanua kwa kifupi!

Kilichotokea ni kuwa aliamua kuachana na siasa, tarehe 28 Julai 2015, majira ya saa tatu usiku, baada ya kuona yanayofanyika ndani ya chama chake hayamridhishi.

======
anasema ukweli na upotoshwaji lazima usemwe,utamkwe na yanayoaminiwa yasemwe.
sina tabia ya kuyumbishwa, nasimamia ninachokiamini. mengi yamesemwa mitandaoni, magazeti na hata na viongozi wenzangu. sina ugomvi, chuki wala hasira na mtu yeyote.

lakini katika nchi kuna misingi inayoongoza taifa. hakuna siasa safi inayokwenda kwa propaganda. matokeo ya propaganda ni vita.

anasema


1.sikuwa likizo
2.sina barua yyte kwamba naenda likizo

ki;lichotokea ni hiki
niliamua kuachana na siasa na kimsingi kazi hiyo ilitokea tr 28 july usiku baada ya kuona yale yaliyofanyika ndani ya chama changu sikufurahishwa...pia

2.kusema Dr Slaa alikuwepo tangu mwanzo kumleta edward lowasa kwenye chama ni uongo.
kwa kifupi sana baada ya tr 11 08 baada ya lowasa kukatwa pale dom mshenga wake lowasa mch.gwajima alinipigia simu kuwa nini kinafuata.
nilimwambia tumsikie mwenyekiti anasemaje...nikamwambia tukutane ofsini.
nilichoshiriki ni kutaka kujua kama atahama ccm au la na pili anapoenda kutangaza ajisafishe na kashfa ya ufisadi wa richmond,

cha ajabu tangu ahame ccm hajatangaza wala kujisafisha

mambo mawili
1.Anayekuja kwako ni asset au liability

binafsi sijatoka chadema kwa sababu ya urais. dr anataka mgombea mwenye sifa, mwenye uwezo na anayeweza kuivusha chadema kuchukua nchi. hata mwaka 2010 sikugombea ila niliombwa.
- tulitaka kujua anakuja na nani, na wenzake, viongozi serious au na vijana wa mitaani.
-tuliambiwa anakuja na wabunge wasiopungua 50, wenyeviti wa mikoa 20 na wenyeviti wa wilaya 100.
- Niliomba majina hayo lakini sikuyapewa. kama katibu mkuu makini nisingekubali kupokea mtu bila kupima kama asset au liability.

====tangu 2004 sijawahi kutofautiana na mwenyekiti wangu mbowe lakini kwa mara ya kwanza tumetofautiana naye katika hili.
kabla ya kamati kuu tulikaa watu wanne mbowe,mimi,lissu na gwajima.
Nilivyoona hivi niliandika barua ya kujiuzulu pale pale lakini ikachanwa na prof safari. nikaandika nyingine kwa makam znz akaniambia haya mambo yamepangwa unajisumbua bure.

2. Propaganda ni nyingi mara dr amefungiwa nyumbani, mara atakuja ofsini kuongea na media.
- sijawahi kuzuiwa na josephine kufanya jambo lolote, lakini kumbeni amewahi kumwaga damu kwa ajili ya ukombozi wa nchi hii, amezunguka nchi hii kila kona.
-silipwi milioni saba kama inavyodaiwa.tunakula mihogo kama watz wengine,tunakula maharage kama watz wengine.

=========cha muhimu
jina la chama tulichokijenga kwa muda mrefu lisiharibiwe
=====jina la uadilifu la mwanasiasa ulilolijenga kwa muda mrefu lisiharibiwe.
hapa tunaangalia credibility

jambo lingine
====Asset ni jambo linalopimika ......hakuna asset tuliyopata kwa lowasa. ni uongo mtupu.kina mahanga walioshindwa huko,sumaye ambaye ni mzigo kabisa ana uchafu wa kutosha, amechukua shamba la magereza huko kibaigwa...huyu huyu sumaye aliyesema atajiuzulu....sumaye ni kapi,lowasa ni kapi. tumekula matapishi yetu.....
msindai ni mzigo, namjua tangu tukiwa bungeni...mgeja simjui siwezi kumsemea.
guninita ni mzigo hata kuandika report hawezi, ni mzigo tangu akiwa uvccm
....wengine wanasema ni muhimu tuiondoe CCM hata kwa kumtumia shetani.. si kweli...unaiondoa ccm kwa program serious, kwa mpango makini.
.....leo lowasa anatufunga mdomo hata haijaisha mmwezi mmoja.

====suala lingine nani hana madhambi....si sahihi
====ccm kinalea matatizo, kimemlea lowasa hadi hapo alipofikia....
-=====ukimuona mtu anahamisha choo kutoka kilipo na kuukihamishia chumbani anakolala utasemaje?? hawa wamehamishia choo chumbani..

tuhuma dhidi ya lowasa
1.tulimwambia atoke hadharani atueleze ukweli wa richmond
msingi wa kwanza wa richmond lazima urudi kwenye taarifa ya mwakyembe...nawashukuru sita na mwakyembe kwa kutoka hadharani kusema hayo, watoke zaidi ya hapo tuwanyamazishe hawa. linihongwa mil 500 nikakataa.

mwanzo wa richmond ni lazima urudi kwenye taarifa ya baraza la mawaziri ya kabla ya taarifa ya richmond.
richmond ilianzia kwa mkapa sio kikwete.
===2006 wakati maamuzi ya richmond yanafanyika waziri mkuu alikuwa lowasa.

===dr slaa anaelezea mchakato mchafu wa upatikanaji na upewaji wa zabuni wa kampuni ya richmond uliosimamiwa na lowasa akiwa waziri mkuu

Dr Slaa anaelezea mchakato mchafu wa upatikanaji na upewaji wa zabuni wa kampuni ya richmond uliosimamiwa na lowasa akiwa waziri mkuu

No comments:

Post a Comment