Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbrod Slaa, Septemba 1, 2015, ametagaza rasmi kuondoka katika chama hicho na kustaafu mambo ya siasa akiwa katika vyama vya siasa nchini Tanzania.
Hata hivyo amesema, ataedneleakuwa Mtanzania na hivyokufanya siasa akiwa mwananchi wa kawaida.
Zifuaazo ni dondoo za hotuba yake, aliyoitoa katikahoteli ya sreena jijini Dar es Salaam, akitangaza uamuazi wake huo
Kutoka Serena Hotel Ambako Dr. Slaa Anaongea
1.Napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutujali uzima.
2. Nimeamua kujitokeza leo hii ili kumesha upotoshaji na kuuweka wazi ukweli.
3.Sina tabia ya kuyumbishwa na ninasimamia ninachokiamini.
4.Sina ugomvi na kiongozi yeyote maana siasa sio uadai.
5. Siasa inapoongozwa kwa misingi ya upotoshaji, matokeo yake ni vurugu.
6. Naweka wazi kuwa mimi sikuwa likizo na hakuna aliyenipa likizo yoyote.
7.Kilichotokea ni kuwa niliamua kuachana na siasa tangu 28.7.2015 saa sita usiku baada ya
kutoridhishwa na kilichokuwa kinaendelea ndani ya chama changu.
8.Ni kweli nilishiriki kumleta Lowassa CHADEMA Lakini nilikuwa na misimamo yangu ambayo ilitufanya
tusielewane.
9. Baada ya Lowassa kukatwa pale Dodoma, Gwajima ambaye ni mshenga wa Lowassa alinipigia simu
kutaka kujua nii cha kufanya.
10. Nilimpigia Mwenyekiti Mbowe kumjulisha na tukakubaliana kupanga muda wa kuwasikiliza.
11. Kabla ya kuanza kuwasikiliza, msimamo wangu ulikuwa ni kumtaka Lowassa kwanza atangaze
kuhama chama, aweke wazi ni chama gani anaenda na ajisafishe juu ya tuhuma zake
12.Tangu akatwe jina, Lowassa hakutangaza kujitoa CCM na wala hakujisafisha na tuhuma zake, kitu
kilichonifanye nitofautiane naye.
13. Niliwauliza wanachadema wenzangu kuwa Lowassa anakuja kama Mtaji au Mzigo?
14. Swala sio urais kama watu wanavyozusha, mimi nilikuwa nataka mgombea mwenye uwezo na sifa
ambaye ataweza kuitoa CCM. Sikuwa na tamaa ya urais kama watu wanavyosema
15. Tangu Gwajima atupe taarifa za ujio wa Lowassa, Swali langu la Lowasssa kuwa Mtaji au mzigo
halikuwahi kujibiwa.
16. Nilitaka kujua ni mtaji gani lowassa atakuja nao na ni viongozi gan atakuja nao.
17. Nilijibiwa kuwa anakuja na wabunge 50 wa CCM, wenyeviti 22 wa mikoa na wenyeviti 80 wa
wilaya.
18.Baada ya ahadi hiyo, nilitaka sasa nipewe majina ya hawa watu lakini mpaka tarehe 25 july
sikupewa hayo majina
19. Wenzangu waliniambia kuwa tarehe 27 niitishe kikao cha dharura ila niligoma kwa sababu nilikuwa
sijapewa haya majina
20. Ndani ya kikao hicho, tulianza kwa mabishano makali kati yangu na Mbowe, Lissu na Gwajima,
viongozi wenzangu ni shahidi na mungu anajua. Msimamo wangu ulikuwa ni uleule kujua mchango wa
Lowassa
21. Kikao kile kikavunjika, baadae tukaingia kamati kuu lakini bado msimamo wangu ulikuwa ni uleule.
Baadae nikaandika barua ya kujiuzulu.
22.Profesa Safari aliichana ile barua.
23.Cha kusikitisha ni kuwa Kesho yake picha zikaanza kusambaa mtandaoni zikimuonyesha la lowassa
japo viongozi wangu walizikana zile picha. Kibaya ni kuwa viongozi waliuficha ukweli
24. Kesho yake niliandika tena barua rasmi ya kujiuzulu.
25. Baada ya pale zikaanza propaganda za uongo zikimuhusisha hadi mke wangu eti kanizuia.
26. Naomba watanzania wajue kuwa mke wangu hakuwahi kunizuia kwa lolote, lkn hata angefanya hivyo
sio mbaya maana hata yeye ni mwanaharakati mwenye uchungu na nchi hii.
27. Mke wangu aliwahi hadi kuumia wakati akipigania ukombozi wa nchi hii.....Lakini sio mbaya, familia
yangu imezoea propaganda.
28. Kikubwa katika harakati ni credibility ambayo lazima uilinde na mimi sitaki jina langu liharibiwe na
ni haki yangu.
29. Maslah mapana ya taifa ndiyo yaliyotufikisha hapa na sio maslahi binafsi.
30.Lowassa na wapambe wake ni waongo maana hakuna hata kipengele kimoja walichokitekeleza.
31. Tulitaka hao wabunge 50 waje kwanza kabla ya mchato wa uteuzi ccm
32. Napinga kuchukua makapi ya CCM kuyaita MTAJI.
33.Mtu kama Sumaye ni FISADI na nilikuwa siongei naye
34. Sumaye aliwahi kusema CCM wakimchagua Lowassa atahama chama. Leo Lowassa kawaje msafi??
35. Tulitaka Mtaji toka kwa Lowassa na sio MAKAPI
36. Wenyeviti walioletwa na Lowassa ni MZIGO na namjua vizuri. Akithubutu kunijibu ntamwaga UOZO
wake wote
37.Nani asiyejua Guninita pia ni mzigo??
38: Nawataka viongozi wangu wanijibu ni mtaji upi walioupata toka kwa Lowassa.
39. Mimi ni Padri Mstaafu, sipendi siasa za uongo.
39. Ukisema unataka kuiondoa CCM ni lazima ujikumbushe misingi ya CHADEMA ambayo ilikuwa ni
uadilifu. Leo chadema hii ina Uadilifu gani??
40. Namshangaa sana Lowassa eti kusimama mbele ya watu akijinasibu kuwa ni msafi.....kwamba
mwenye ushahidi aende Mahakamani. Ni dhambi kupotosha watu.
41. CCM hawana ujasiri, ni waoga na ndiyo maana wamewalea watu kama akina Lowassa
42. Ukitoa kinyesi chooni na kukipeleka Chumbani maana yake hata chumba chako ni CHOO na
kitakuwa kinanuka zaidi kulicho choo cha kawaida
43.Mimi nilikuwepo wakati sakata la Richmond likijadiliwa.Mimi nina ugomvi wa muda mrefu na
Lowassa.
44. Mwaka 2010 mimi nilimtaka Lowassa atangaze Richmond ni ya nani.
45. Leo tena namtaka Lowassa namtaka Lowassa atoke hadharani atangaze Richmond ni ya nani.
Unaposema ni ya mkubwa, atuambie mkubwa gani
46. Ukitaka kuijua Richmond rejea Ripoti ya Mwakyembe. Nampongeza Mwakyembe na Sitta kujitokeza
hadharan kuusema ukweli.
47. Siku moja kabla ya ripoti kusomwa, nililetewa Rushwa ya milioni 500 ili tukaupindishe ukweli
bungeni lakini nilikataa
48. Ripoti ya mwakyembe iliamua mambo mawili, moja; Lowassa ajipime au bunge lijadili na lichukue
ripoti. Lowassa kuona hivyo akaamua kukimbilia kujiuzulu kukwepa aibu ya kung'olewa na bunge
49: Lowassa haaminiki, ni muongo na hastahili kuwa Rais wa nchi....
50. Lowassa ni FISADI na kama mimi ni muongo ajitokeze hadharani akanushe
51. Anasema Lowassa ataleta maji, mbona jimbo lake la Monduli halina Maji???
52. Mnasema Lowassa kaanzisha shule za kata, iv mjua msingi wa shule za kata? waandishi rudini
shule mkajifunze upya.
53.Nilifanikiwa kuijenga Chadema na ikawa tumaini jipya la watanzania.....Vijana wangu wa Chadema,
naomba niwe mkweli propaganda imekivamia chama.
54. Inasikitisha kuona CHADEMA inajaza mabasi pale jangwani badala ya watu.....alafu mnawadanganya
watu eti ni MAFURIKO
55. CHADEMA ya kipindi changu ilikuwa inakemea Rushwa. Niambien leo chadema watasema nini
kwenye majukwaa?
56. Mnaomtetea Lowassa na nyie jitokezen hadharani...mimi nasema kwa sababu nina ushahidi na sio
lazima ushahidi huu niupeleke mahakamani.
57. Wenye uwezo wa kumpeleka Lowassa Mahakamani ni Serikali, na mwakyembe alisema juzi kuwa
kesi ya jinai haina kikomo, mtu anaweza kushitakiwa muda wowote
58. Sitaki kuingila swala la Babu Seya, lakini waliolawitiwa ni watoto waliokuwa chini ya umri. kwa nini
haki yao ipotee?
59. Rais hana mamlaka ya kumtoa Babu Seya. Lowassa asiwadanganye.
60. Kuhusu swala la Masheikh, Sumaye ndiye aliyeamuru mapolisi wavamie misikiti wakiwa na
mbwa......Watanzania msikubali kudanganywa. hizo ni propaganda za wasaka urais
61. Masikubali Rais Muongo na mimi naapa ntapiga kelele kila kona kumpinga Lowassa.
62.Lowassa alipokuwa waziri mkuu, matatizo yanayotokea leo hayakuwepo? mapigano ya wakulima na
wafugaji hayakuwepo?
63. Lowassa akiwa waziri mkuu alisababisha migogoro mizito sana kati ya monduli na karatu. Rais wa
aina hii wa nini?
64. Naomba nisiongee mengi kwa sababu ntakosa ya kusema siku nyingine.....Nawataka Lowassa na
Sumaye wajitokeze kunijibu.
65. Siku nyingine ntakuja kuongelea kuhusu hisa za Lowassa kwenye makampuni
66. Nahitimisha kwa kusema kuwa Nimestaafu siasa na sina chama lakini nina nchi, hivyo ntaendelea
kuwatumikia watanzania kwa jinsi mungu alivyonipa vipawa
67. Narudia tena, Sina chama na sitajiunga na chama chochote.
No comments:
Post a Comment