Meja jenerali Prime Niyongabo, Mkuu wa majeshi ya Burundi ameponea kuuawa katika shambilo lililoendeshwa dhidi ya gari lake leo Ijumaaa asubuhi Spemba 11 wakati ambapo alikua akijielekeza kazini.
Na RFI
Mkuu wa Majeshi ya Burundi Meja jenerali Prime Niyongabo ameponea kuuawa katika shambulio la roketi liliyolenga gari lake. Inaarifiwa kuwa watu waliokua wamevalia sare ya jeshi wameshambulia gari la mkuu wa majeshi ya Burundi karibu na daraja la Muha wilayani Kinindo.
Shambulio hilo limetokea leo Ijumaa saa 12:45 (saa za Afrika ya Kati). Inaarifawa pia kuwa wanajeshi kadhaa wameuawa katika shambulio hilo.(P.T)
No comments:
Post a Comment