Friday, September 18, 2015

UKAWA WAZIDI KUJICHANGANYA MBOWE SASA AMUANGUKIA DR. SLAA HABARI KAMILI YA KWANZA

Petro Magoti
MBOWE ASALIMU AMRI KWA DR SLAA.AMFATA ULAYA KIMYA KIMYA.

Baada ya mwenendo wa Kampeni kuonekana kuwa mgumu huku kila alichoahidi Lowassa kutotimia mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe aamua kukutana na aliyekuwa katibu wake Dkt. Wilbroad Slaa nchini Marekani.

Taarifa za uhakika ni kuwa Mbowe aliondoka nchini toka juzi na kupokelewa na wanachama wa Chadema tawi la DMV aliposhuka Uwanja wa Kimataifa wa Dulles huko Marekani ambapo Dkt. Slaa alimtangulia muda kidogo.


Taarifa zilizopatikana toka kwa moja ya viongozi wa tawi hilo aliyejulikana kama Kalley Pandukizi amesema ni kweli Mbowe na Slaa tumewapokea na wapo hoteli moja hapa Ohio kwa ajili ya mazungumzo binafsi. Amekiri baada ya kumpokea Mwenyekiti wao Mh. Mbowe walimpeleka moja kwa moja hotelini ambapo ndipo walipomkuta Dkt. Slaa.



Tetesi zaidi zinasema Mbowe amemuomba msamaha sana Dkt. Slaa na kumueleza walipotoka kwani mgombea waliomchukua anadhoofika kiafya kila kukicha kiasi kwamba mikutano mingine wananchi hawamsikii anapohutubia vile vile hakuna hata moja alilotimiza katika makubaliano kabla hatujampokea zikiwemo fedha za kampeni hivyo chama kinapata wakati mgumu wa kufanya kampeni kikamilifu.

Inasemekana Mbowe amemueleza Slaa kuwa ujio wa Lowassa umeigharimu Chadema kwani mpaka sasa John Mnyika hajakubali kupanda majukwaani kumnadi Lowassa kitu ambacho ni tabu zaidi kwao. Pamoja na vijana wa Lowassa kuuteka mchakato mzima wa kampeni hali inayokiuka makubaliano tuliyompa.

Kikubwa ni kuwa taarifa za ujumbe mfupi toka kwa Bi. Helen Ongara ambaye ni katibu wa BAWACHA tawi hilo la DMV ni kuwa Mwenyekiti huyo amepoteza tumaini hasa alipowapa video ya Mgombea akiomba kura kwa kigezo cha ulutheri kimewagharimu zaidi hivyo amedai watapigana ili wapate viti vya ubunge ila urais watapoteza.

Hata hivyo aliwadokeza kuwa kampeni zinaratibiwa na Lissu lakini wanafikiria kuchukua maamuzi magumu ya kuwatosa UKAWA ili wabaki wao kama wao kuliko sasa ambapo wanavibeba vyama vya NCCR MAGEUZI, NLD na CUF. Ambapo hata hivyo hali ya mpasuko imeanza kuonekana kupitia vyama vya CUF na NCCR MAGEUZI.

No comments:

Post a Comment