AMANI IWE JUU YENU ENYI WAJA WEMA WA BWANA MUNGU WANGU...!!

Katika muendelezo wa kuwafikirisha, nimeona leo niwaandikie kuhusu hali ya Upinzani na kampeni zinavyoendelea hapa nchini, ambapo hali ya sintofahamu ikiendelea kudhirihi kwa CHADEMA na Kambi yote ya Upinzani hapa nchini, wachambuzi mbalimbali, wasomi na waandishi wameendelea kuandika wakijaribu kuonyesha tatizo lililoikumba kambi hiyo, wengi wao wakisema FEDHA, vipande vya rupia vilivyoingia CHADEMA vimewafarakanisha. Nami Binafsi ktk muendelezo huo huo wa kuchambua hali hiyo nitaeleza CHANZO ama SABABU halisi ya SINTOFAHAMU inayoikumba kambi ya Upinzani.

Kwa Muhtasari sana, niseme CHANZO na SABABU HALISI ya Upinzani kukosa muelekeo na kufikia hapa tulipo ni OMBWE la UONGOZI katika kambi hiyo ikiongozwa na CHADEMA..Mimi niliwahi kuwa mwanachama wa CHADEMA, tena Kiongozi Mkubwa katika jumuiya yake ya Vijana, nilipata fursa ya kushiriki, kuhudhuria na kuchangia katika vikao na mikutano mikubwa, muhimu na nyeti ya Chama hicho.

Ilikuwa bayana kwetu kuwa, ilipofikia CHADEMA ilihitaji UONGOZI mpya utakaokuja na dira, maono na tafakuri mpya ambayo ingeki-transform chama hicho kuwa chama kamili cha siasa na kuondoa uongozi wa hamasa na mihemko ya kiuanaharakati..

Nikiwa ndani ya Vikao vya CHADEMA nikaliweka hili BAYANA kuwa tunalo ombwe la uongozi ndani ya CHADEMA, sikueleweka, nikaonekana natishia maslahi ya wakubwa na nafasi zao kwenye Chama, nikaonekana ADUI na nikapewa jina MSALITI.

Ukweli ni kwamba FEDHA ambayo leo imetajwa mara kadhaa kuwa ndio sababu kuu ya mfarakano ndani ya CHADEMA, imepata njia kutokana na Ukweli kuwa CHADEMA kuna Ombwe la Uongozi ambao umekosa Vision na Mission, ndio maana wakadhani FEDHA na UMAARUFU wa mtu ni mtaji wa wao kuingia Ikulu, wakasahau misingi, dhamira, imani na kiu ya Watanzania.

CHADEMA haina tabia ya kujitafakari, haijisahihishi, na wamezoea kuishi kimazoea, wanadhani kila siku ni jumapili na kila walisemalo watanzania watalikubali tu madhari limesemwa na wao, na kwamba kila muongeaji basi anasikilizwa. SIO HIVYO...!!

Leo waongeaji wa CHADEMA na WATETEZI wakuu kwenye mitandao ni YERICKO NYERERE, A man with 0.001 IQ, Anaishi katika uongo na uzushi, mpaka kila mmoja amemmpuuza, Mwanakijiji, Chahali na WATABE wengine wa maandishi yenye adili, wameikacha CHADEMA, bado CDM haijiulizi, inajivunia kuwa na YERICKO. Wasomi, watumishi, na wanataaluma wameikacha CHADEMA, bado CDM haijiulizi, wanajivunia madereva bodaboda.

Moja ya sifa ya Mwerevu, ni yule ambae haumwi na nyoka mara mbili, anayejikwaa akaanguka kisha asiishie kuangalia alipoangukia bali hugeuka kwa umakini na kutazama alipojikwaa, ni nini hasa kimemuangusha..Popularity ya CHADEMA na Upinzani imeshuka na inaendelea kushuka kwa kasi, HAWAJIULIZI.

Viongozi wameacha kuchangia hoja za msingi ndani ya Vikao, wameshikwa na woga na wengine wamesusa, Mwenyekiti Mbowe ambae Mimi binafsi nilishamuita ZERO tukiwa ndani ya Kikao changu cha Mwisho nikiwa KAMANDA wa CDM, ameendelea kwenda Mrama kwa kasi ya ajabu...kila jipya analoliamua ni baya kuliko la jana..