Friday, September 4, 2015

LOWASSA ANGANI VS MAGUFULI ARDHINI




Wakati mgombea urais wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, ameanza harakati za kuomba kura kwa wananchi kwa kutumia helkopta (Chopa) baada ya kuchoka na kudhoofika kwa kutumia usafiri wa ardhini, mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, ataanza kuuteka Mkoa wa Morogoro leo kwa staili ile ile ya kutumia Magari. 

Lowassa ambaye ameanza kampeni mikoani Jumamosi iliyopita alikuwa akitumia usafiri wa magari, huku kwa siku alifanya kati ya mikutano miwili hadi mitatu. Mikoa ambayo hadi jana mgombea huyo na msafara wake walikuwa wamefanya mikutano ya kampeni ni Iringa, Njombe, Rukwa na Katavi. Leo Lowassa yupo mkoani Kigoma ambapo atakuwa anatumia usafiri wa Helkopta. 

MAGUFULI ARDHINI Baada ya siku kumi za milima, mabonde, barabara za lami, vumbi, njaa, jua, manyunyu ya mvua, za kutembea takribani kilomita 4,000 kutoka Dar es Salaam hadi Katavi na kuelekea Mtwara kukamilisha ngwe ya kwanza, mgombe wa urais wa CCM, Dk. Magufuli, amefanya takribani mikutano 80. Zilikuwa siku za kupata ajali ndogo, magurudumu kupungua upepo na baadhi ya magari kubaki nyuma, wakati mwingine kupotea njia baada ya kuachwa. Kazi hiyo leo imehamia mkoani Morogoro kwa mgombea huyo kutafuta ridhaa ya wananchi kumpigia kura za kutosha zitakazomwezesha kuingia Ikulu Oktoba 25, mwaka huu. 

Mh. Magufuli anaonyesha uimara wa kuwa Head of State kwa kwenda kila Kata, Jimbo, Wilaya na Mkoa kwa kutumia usarifi wa ardhi. Huyu ndie Mgombea anaye weza kuiongoza Tanzania. Mungu Mbariki Mh. John P. J. Magufuli.

No comments:

Post a Comment