Baadhi ya vijana wa Chadema mkoani Mwanza wakichana kadi za Chadema
Vijana kutoka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Mwanza wameandama pamoja na kuchana kadi, kuchoma bendera ya chama hicho kwa madai ya kuchukizwa na kitendo cha Katibu mkuu Dr.Wilbdroad Slaa kutangaza kujiuzulu cheo chake na kuachana na masuala ya siasa.
Wakizungumza wakati wa maandamano hayo vijana hao wamedai kukasirishwa na kitendo cha Dr.Slaa kuhama chama hicho kwa madai ya kumpokea Edward Lowassa na kumpitisha kugombea urais kwa kupitia umoja huo kwa madai ya kuhusika na kashifa ya ufisadi iliyopelekea ajiuzulu mwaka 2008.
Hata hivyo, uamuzi wa Dr.Slaa kuachana na masuala ya kisiasa umepokelewa kwa namna tofauti huku Mwenyekiti wa Chama cha Chadema Freeman Mbowe akidai kuwa chama cha Chadema sio mali ya mtu mmoja na kusisitiza chama hicho ni kama treni ambayo wapo watao panda na wengine kushuka.
No comments:
Post a Comment