Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, akizungumza na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, kuhusu nafasi na majukumu yao katika uchaguzi mkuu, pamoja na jinsi Serikali ilivyojipanga kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani, huru na haki kwa vyama vyote.
Waheshimiwa Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, wakati wa mkutano huo uliofanyika jana 10-09-2015 katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIC) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Maharage Juma, akiwatambulisha Mabalozi waliowasili nchini hivi karibuni ambao ni mara yao ya kwanza kuhudhuria Kikao cha aina hii, Wizara ya Mambo ya Nje.
Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini Mhe.Thamsanga Dennis Mseleku akiuliza swali katika mkutano huo.(P.T)
No comments:
Post a Comment