Saturday, September 19, 2015

MBOWE ASEMA TUKUTANE 2025 KUENDELEZA HARAKATI


WATANZANIA WACHACHE WAOGA KUFIKIRI

Na Thadei Ole Mushi.
Asante Dr Slaa sisi vijana ambao tumetumia kodi za taifa hili kutulea kiafya, kijamii na Kielimu tumekuelewa sana ulichokiongea. Hakuna ubishi baada ya mwalimu Nyerere kututoka nadhani viatu vyake kuhusu maslahi ya Taifa hili vimekuenea vizuri sana.

Kuanzia miaka ya 1650 bara la Ulaya lilipitia kipindi muhimu sana ambacho kimelifanya bara hilo kufikia hapo lilipo hivi leo kimaendeleo. Katika miaka hiyo ambayo ni katikati ya karne ya 17 bara ulaya liliingia kwenye kipindi kinachojulikana kama “age of Enlightenment” au “Age of Reason”. Katika kipindi hiki watu wa bara hili waliamua kufanya mambo kwa kufikiria. Kipindi hiki kilibadilisha kabisa maisha ya bara hili na kulifanya kuendelea. Ulikuwa ndio mwanzo wa kuibuka kwa philosophers wengi tunaowasoma leo na kuwaheshimu.


Nani asiyewakumbuka wanafalsafa hawa walioibuka kipindi hicho kama kina Alessandro Volta na Luigi Galvani waliochangia sana maendeleo ya sayansi Italy, nani asiyemkumbuka Voltaire na Jean-Jacques Rousseau, hawa walichangia sana kubadilisha mazoea ya Wafaransa na baadhi ya mataifa ulaya kuachana kufanya mambo kwa kuongozwa na dini hasa ya Kikristu na kuchangia sana watu kuanza kufanya mambo kwa kufikiri kisayansi na kufanya majaribio. Unapozungumzia Mapinduzi ya kisiasa ya Ufaransa hawa watu walioamua kufikiri (Voltaire na Jean-Jacques Rousseau) huwezi kuwakwepa kuwataja. Kule Urusi walitumia kipindi hiki Kutoa wanasayansi wanaoheshimika sana duniani kama kina Leonhard Euler, Peter Simon Pallas, na wengineo. Kwa kifupi hakuna taifa la Ulaya halikunufaika na Kipindi hiki ambacho watu waliamua kufikiri badala ya kuongozwa na Mahaba ya Dini zao, Kabila zao, au hata Vyama vyao. Kipindi hiki ni kipindi pia cha kukumbukwa sana na taifa GREECE kwani walikitumia pia kipindi hiki kujenga miji mikubwa kumbuka “Ottoman Empire”.

Wakati wenzetu wakifikia kipindi hicho cha kufikiri na kuacha kufanya mambo kimazoea 1650 huku kwetu 2015 bado tumejifunika blanketi zito na tumelala fofofo kabisa. Watanzania hasa baadhi ya vijana hawataki tena kufikiri wanataka maisha ya rahisi rahisi sana. Uchaguzi huu unanifanya nifahamu baadhi ya watu hasa baada ya Leo Dr Slaa kuongea. Vijana wachache sana na hawa naweza kuwakadiria wamezaliwa kuanzia miaka ya 1990s wamekuwa wepesi sana kudanganyika. Kwenye uchaguzi huu wamekuja na hoja ya Mabadiliko ila nimewagundua wengi hawajui dhana ya mabadiliko ni nini.

MABADILIKO NI NINI?
Mimi nimeamua kufikiri, Nimeamua kuachana na hili kundi lililofaulu kwa kutumia vitabu vya uchambuzi wa maswali ya NECTA, nimeamua kufikiri kwa kuwa najiamini naweza kufikiri nimesoma maana ya mabadiliko nayajua. Nimesoma ya pande zote nimefungua sana Kurasa za Das Capital ya Carl Max na mawazo ya kibepari (bourgeoisie conception) hawa wote kwa nyakati tofauti walikuwa wanahitaji mabadiliko hata leo taifa la Marekani Linahitaji mabadiliko Kwa kuwa linahitaji kutoka sehemu moja iliyo bora kwenda Iliyo bora zaidi.Wamarekani hadi leo hawajalala wanafanya kazi usiku na mchana kufikiri ni namna gani wataendelea kuitawala dunia, Hawa wameamua kufikiri.

Mabadiliko ni kutoka sehemu moja mbaya kwenda sehemu nyingine iliyo bora zaidi, Hii ni maana rahisi sana inayoendena na mazingira chanya ya mabadiliko. Je watanzania kupitia uchaguzi huu kweli tumefikiri na kuamua aina ya mabadiliko tunayoyataka?. Kama una muda hebu pitia “Anatomy of Revolution” soma hatua za mabadiliko kweli haya ya Lowassa na Sumaye ndio Mabadiliko tunayoyataka? Mimi nikiri naona giza Mbele inabidi tufikiri tusiende tu, Nimegoma kwenda nimegoma kuwa zezeta kama dr Slaa nimegoma kuwa shabiki wa siasa nataka kulikomboa taifa langu kwa mabadiliko chanya ila si haya wanayoimba hawa vijana. Sitaki kuendelea kufikiri zaidi naona madhara ya watu kuhudhuria shule badala ya kwenda kujifunza. Dah kumbe Richmond ni stationary my God hatuwezi kutoka hapa tulipo kwa fikra hizi.

Thadei Ole Mushi

No comments:

Post a Comment