Silaha zilizokamatwa zikioneshwa kwa wandishi wa habari.
Na Timu ya Uwazi, Mkuranga-GPL
HOFU kubwa imetanda kwenye Kijiji cha Mamndi Mkongo kilichopo Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani kufuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na wale wa mkoa huo kunasa silaha nyingine za kivita zikiwa zimefukiwa kwenye shimo msituni.
Tukio hilo la unasaji wa silaha lilifanikiwa Agosti 29, mwaka huu katika msitu mmoja uliopo katika kijiji hicho kilichopo umbali wa kilomita 23 kutoka mjini Mkuranga.
NI KAWAIDA YA UWAZI
Baada ya Uwazi kuzipata taarifa za polisi kuzinasa silaha hizo lilifunga safari hadi kwenye eneo la tukio na kushuhudia shimo ambalo silaha hizo za kivita zilifukiwa kwa utunzaji wa siri.
Silaha za kigaidi zilizokamatwa.
MKUU WA MGAMBO ASIMULIA
Katika Mahojiano maalum na kiongozi wa wanamgambo wa Kata ya Bup iliyopo kwenye kijiji hicho, Mussa Mohammed Koti alisema wamekuwa wakifanya doria katika mazingira magumu na hasa baada ya vikosi vilivyokuwepo kuondoka. Awali huku kulikuwa na vikosi maalum vya ulinzi na usalama.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akizungumza na wandishi wa habari.(P.T)
No comments:
Post a Comment