Sunday, September 20, 2015

CHADEMA NA CUF ZAPAMBANA BUKOBA


Chama cha Wananchi (CUF) wilaya ya Bukoba Vijiji, kimekishtuma Chama cha Demokrasia na maendeleo- CHADEMA- mkoa wa Kagera, kwa kukiuka makubaliano yaliyofikiwa na UKAWA, baada ya kumsimamisha Mgombea Ubunge kinyume na makubaliano.

Shutuma za CUF dhidi ya CHADEMA zimetolewa siku chache baada ya Chama kingine, ambacho ni washirika wa UKAWA, NCCR MAGEUZI kuishutuma CHADEMA kwa kukiuka makubaliano katika mchakato wa uchaguzi mkuu.

Akizumgumza na Waandishi wa Habari, Mgombea Ubunge kupitia CUF, Buberwa Ephrahim Kaiza amesema kuwa CHADEMA wamekiuka makubaliana baada ya kusimamisha mgombea kwenye jimbo hilo kinyume na makubaliano.

Amedai kuwa mgombea wa CHADEMA, Rutashobya Cyliacus Rutashobya anazunguka katika jimbo hilo na kuwaeleza wananchi kwamba hakuna Ukawa, huku Viongozi wa CHADEMA mkoa wakiwa kimya na kuendelea kumunadi licha ya kufahamu kwamba hakupitisha na UKAWA.

No comments:

Post a Comment