Mechi 5, points 15, magoli 13, kufungwa 1 tu. Safari hii naona wale "MAJIRANI WAPIGA KELELE" wamekaa kimya kabisa, ni ishara kwamba wameukubali mziki wa Jangwani, husikii wakisema Tigo Pesa, M-Pesa wala CRBD Bank.

![]() |
Mheshimiwa Sophia Simba leo akiwa mjini Dubai amekanusha habari za UKAWA kwamba anakusudia kujiunga na Chama hicho Tarehe 5/10/2015 kwenye mkutano wanaoutayarisha kufanyika Mwanza ambapo inasadikiwa kwamba Mzee Kingunge na Juma Mwapachu wanategemewa kujiunga na UKAWA. Pia UKAWA walikuwa wamelikisha habari za Dr. Mwakyembe, Mwandosya, Dr. Nchimbi kwamba watajiunga na Chama hicho siku hiyo ya Jumatatu, lakini Viongozi hao wa CCM wote wamekanusha kujiunga na Chama hicho ambacho Dr. Nchimbi amekiita ni Chama kinachoelekea kufa tayari. |
![]() |
Mwenyekiti wa Wazazi/CCM Mkoa wa Dodoma, akiongoza ujumbe wa Kamati ya ushindi ya Jumuiya hiyo ya Wazazi kumtafutia kura Magufuli mkoani Tabora. |