Monday, October 26, 2015

NIONAVYO LEO NI KAMA JANA; SERIKALI YA MAGUFULI INAKUJA..

0_f0836.jpg

Ndugu zangu,
Tusihangaike sasa kujiuliza kama Serikali ya John Magufuli inakuja au la, bali, Watanzania tuanze kujiuliza; " Tumejiandaaje na Serikali ya John Magufuli inayokuja?"
Maana, kwa kuyasikia leo matokeo ya Mara na Tabora, Nyamagana na Ilemela. Hivyo, inahusu Kanda ya Ziwa. Na kwa tulio na uzoefu kidogo wa chaguzi zetu hizi, tunajua, kuwa Kanda ya Ziwa ni ' Political Battle Front'.
Historia ni mwalimu mzuri, anayeshinda Kanda Ya Ziwa ana nafasi kubwa sana ya kupata ushindi wa jumla.
TANU ilianza kuamini kuwa Uhuru wa Tanganyika unakuja pale ilipoweza kujihakikishia kuungwa mkono kwa wingi na Kanda ya Ziwa. Baada ya mafanikio ya Kanda ya Ziwa, kuna wakati, Julius Nyerere alitamka; " We had won the battle by 1957". Ni mwaka huo na uliofuata TANU ilijiwekeza sana Kanda ya Ziwa.
Na unaposikia leo kuwa John Magufuli ametoa upinzani wa kutosha kwenye ngome ya Chadema Arusha na Kilimanjaro, basi, katika siasa, ungelikuwa wakati uliowadia, wa wapinzani wa John Magufuli kwenye kuwania Urais, kuanza kumpigia simu za kumpa pongezi za ushindi. Hakuna namna nyingine bali kuyapokea matokeo hayo yenye kutokana na hali halisi on the battle front.
Mimi nachukua fursa hii kumpongeza kwa dhati John Pombe Magufuli wa CCM kwa ushindi wake utakaotangazwa rasmi wakati wowote kuanzia sasa.
Maggid, http://www.mjengwablog.com/

No comments:

Post a Comment