Katika mashindano ya Urais, kuna mshindaji na mshindwaji. Sasa basi, katika shindano letu la Dkt Magufuli na Lowassa, lazima atatokea Mshindwa, na mshindwa aliye komaa kisiasa atakuwa tayari kukiri kushindwa kwake. Lakini katika hili shindano, teyari kumeanza vuguvugu la mshindwa fulani kupinga matokeo baada ya kuona Majimbo yake ambayo yalikuwa ni ngome yake, yamesha hesabiwa na bado anafuatia nyuma.

Watanzania, tujifunze kushindwa kama ambavyo John McCain wa Arizona alipo concede kushindwa kutoka kwa Baraka Obama kwasababu, ushindani wao ulikuwa ni kulinda Marekani kwanza na sio kukimbilia Ikulu.

Mr Chin