Monday, August 31, 2015

MAMA SAMIA SULUHU ASEMA CCM KUONDOA KODI ZISIZO NA MSINGI NA ELIMU BURE HADI FORM FOUR


Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Babati Mjini.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Babati Mjini.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kushoto akihutubia wanaCCM na wananchi babati Mjini.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kushoto akihutubia wanaCCM na wananchi babati Mjini.
Mbunge anaemaliza muda wake jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba kabla ya mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kupanda jukwaani kunadi sera za CCM.
Mbunge anaemaliza muda wake jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba kabla ya mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu kupanda jukwaani kunadi sera za CCM.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
Na Joachim Mushi, Mbulu
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu amesema chama hicho kikichaguliwa na Watanzania kuunda Serikali tena kitahakikisha kinaweka utaratibu mzuri utakaomfanya mwananchi mfanyabiashara kupenda kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo. Samia ametoa ahadi hiyo Mjini Mbulu alipokuwa akiwahutubia wananchi na wanaCCM katika mkutano wa hadhara wa kampeni za chama hicho.
Alisema watahakikisha wanaondoa kodi za hovyo hovyo ambazo zimekuwa zikitozwa hivi sasa katika maeneo anuai. “…Tutaweka utaratibu mzuri ambao utamfanya mwananchi apende kulipa kodi, ila kodi za hovyo hovyo tutaziondoa…,” alisema mgombea huyo mwenza wa urais akiilani ilani ya CCM na kumuombea kura mgombea urais wa chama hicho, Dk. John Pombe Magufuli.
Akihutubia mkutano mwingine Jimbo la Babati Mjini Bi. Suluhu alisema serikali itakayoundwa na Chama Cha Mapinduzi ili kuboresha sekta ya elimu itahakikisha inatoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne jambo ambalo pia litawapunguzia mzigo familia na kutoa fursa sawa ya elimu ngazi ya msingi na sekondari (kidato cha nne).
Aidha alisema serikali itakayoundwa na CCM pia itahakikisha inafanya maboresho makubwa katika sekta ya afya, umeme, huduma za maji safi na salama pamoja na kuwawezesha wananchi hasa makundi ya vijana na akinamama. Alisema katika maeneo ya wafugaji watahakikisha wanashirikiana na halmashauri kupima na kuweka mipaka ya ardhi katika vijiji ili kuondoa mvutano wa wakulima na wafugaji.
Kuwasaidia wafugaji kujenga majosho ya nifugo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanda vya kuchakata bidhaa za mifugo kuziongezea thamani. Hata hivyo aliwahakikishia wanavijiji ambao wamekumbwa na ukame kuwa Serikali imejipanga kuwasaidia hivyo hakuna mwanakijiji atakaye kufa kwa njaa.
Pamoja na hayo alisema Serikali ijayo ya CCM ili kuongeza kasi ya uwajibikaji imepanga kuunda kitengo maalumu cha kupokea na kushughulikia kero na malalamikoa ya wananchi, jambo ambalo litaweka bayana nani hataki kuwajibika kazini.

CCM JIMBO LA KAWE YAZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU YAMNADI KIPPI WARIOBA

Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (katikati mbele), akisindikizwa na wanachama wa chama hicho, alipowasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati CCM ilipozindua kampeni kwaajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana. 
PICHA/JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge (kulia) akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni kwaajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’ (kulia) akimpongeza Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba baada ya kumkabidhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’ (kushoto) akimtambulisha Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba baada ya kumkadhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana.


Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (kulia), akiusalimia umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, baada ya kutambulishwa na kukabidhiwa Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Katibu Mwenezi wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’.
Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akizungumza umati wa wanachama wa CCM na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam jana.
Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akiinadi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana.
MAMA MZAA CHEMA … Mama Evelyne Warioba ambaye ni mama mzazi wa Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akiusalimia umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. 
Sehemu ya umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. 
Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa akimwaga sera za CCM mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi huo. 
Mhamasishaji maarufu kwa jina la ‘Msaga Sumu’ naye alikuwepo

VITUKO VYA UCHAGUZI!! HUYU HAPA MGOMBEA ALIYEWAPATANISHA WAKE ZAKE JUKWAANI

KUHUSU RICHMOND LOWASA NA MWAKYEMBE NANI ANASEMA UKWELI NA NANI ANASEMA UONGO? SIKILIZA HAPA VIDEO LIVE!!




Sababu 10 kwa nini John Magufuli atashinda uchaguzi Mkuu wa Urais 2015






Sababu 10 kwa nini John Magufuli atashinda uchaguzi Mkuu wa Urais 2015

1.       Tanzania bara na visiwani yako majimbo ya uchaguzi 266, CCM imesimamisha wagombea Ubunge katika majimbo yote 266 huku Chadema na washirika wake wa Ukawa wakiwa wamesimamisha wagombea katika majimbo 211 (138 toka Chadema). Kati ya majimbo hayo 266, CCM tayari imepita bila kupingwa majimbo 7. Ukichukua majimbo 259 yaliyobaki na kutoa 211 ambayo Chadema na washirika wake wamesimamisha wagombea unabaki na majimbo 48 ambayo CCM haina upinzani wa Chadema wala washirika wake wa Ukawa. Majimbo haya 48 CCM ina uhakika wa kushinda walau kwa asilimia 90, ushindi huu si kwa Wabunge tu bali pia kwa mgombea Urais wa CCM.


2.       Watanzania waliojiandikisha kupiga kura mwaka 2015 ni milioni 24.2. Takwimu zinaonyesha CCM ina wanachama hai wapatao milioni 8 wenye kadi na wanaolipia ada zao za uanachama kila mwaka.  Kuondoka kwa Edward Lowassa katika Chama Cha Mapinduzi kunamaanisha Magufuli hatapata kura zote milioni 8 za wana CCM na pia kihesabu si rahisi wana CCM wote milioni 8 kujitokeza siku ya kupiga kura. Utafiti unaonyesha kwamba wana CCM watakaopiga kura hawatazidi asilimia 90 ya wanachama wake (milioni 7.2) huku milioni 7 kati yao wakimpigia kura John Magufuli. Historia ya CCM inaonyesha ni wanachama wachache sana humpigia kura kada mwenzao anapohama kugombea nafasi kwa chama kingine, hasa nafasi ya Urais (Rejea: Uchaguzi wa Urais 1995, mgawanyo wa kura za Augustine Lyatonga Mrema)


3.       Mizunguko ya kampeni huzaa kura za ziada mbali na zile za wanachama. Tayari inaonyesha kwamba Magufuli anapita karibu kila kata ya Tanzania akitumia barabara huku upande wa Lowassa na shirikisho la Ukawa hali ikiwa tofauti, ambako amekuwa akifika sehemu chache akitumia usafiri wa ndege na helkopta na ni wazi hana stamina ya kuzunguka kwa gari nchi nzima kutokana na tatizo la kiafya.  CCM ina mizizi kwenye mashina kuanzia ngazi ya nyumba kumi. Mtandao huu wa Chama pamoja na safari za mgombea wao kila kata ni kiashiria kwamba atafikia wapiga kura wengi zaidi hasa sehemu za vijijini na ambazo si rahisi kufikika. Tafiti zinaonyesha huko ndiko kwenye wapiga kura wengi na kuwafikia ni hatua moja kuelekea kuzipata kura zao na kushinda. 

4.       Chaguzi za Serikali za Mitaa mwaka 2014 zinaonyesha kwamba CCM ilishinda kwa zaidi ya asilimia 80 kwenye nafasi za uongozi za serikali za vijiji na mitaa. Ikumbukwe kwamba CCM ilipata ushindi huu licha ya ushindani mkubwa uliokolezwa na sakata la Escrow wakati huo. Hii inaonyesha kwamba CCM iliweza kushinda hata wakati huo wa changamoto. Ni mwaka mmoja tu umepita tangu chaguzi hizo zifanyike. Kitafiti, hiki ni kiashiria kikubwa kwamba katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, CCM kama chama kinaenda kwenye sanduku la wapiga kura kikiwa na rekodi nzuri kuweza kushinda.



5.       Rekodi ya Utendaji ya Magufuli inavutia Watanzania wengi. Utafiti unaonyesha kwamba wapinzani wake majukwaani mpaka sasa wanapata wakati mgumu kutaja jina lake moja kwa moja kumuhusisha na utendaji wa hovyo. Mitandaoni zipo video na nukuu nyingi zikiwemo za Mgombea wa Ukawa Edward Lowassa, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wengineo wakisifia utendaji wa Magufuli. Katika siasa na kampeni, hatua moja kuonyesha mgombea anashinda ni kushindwa kwa wapinzani wake kumnyooshea kidole moja kwa moja au kukosa mabaya ya kusema dhidi yake. Asiye na la kukusema vibaya anawapa wananchi nafasi ya kuona mazuri yako na kushinda.

6.       Suala la afya ya wagombea limekuwa gumzo kubwa katika uchaguzi wa mwaka huu. Huku ikiwa wazi kwamba Mgombea wa Ukawa Edward Lowassa anaugua ugonjwa wa Parkinson’s kwa muda mrefu sasa, Magufuli hajawa na changamoto ya afya. Ugonjwa wa Parkinson’s alio nao Edward Lowassa unaathiri ubongo wa kati, moyo, mishipa ya fahamu na uwezo wa kufikiri  (Afya ya mwili maeneo hayo ni muhimu kiongozi kuwa nayo). Kwa muda mrefu Lowassa amekuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa huu katika hospitali maarufu ya Franziskus-Krankenhus mtaa wa Budapester jijini Berlin, Ujerumani.  Kiumri Magufuli ana miaka 55 huku Lowassa akiwa na miaka 63. Wapiga kura huchagua kiongozi kwa kutazama muonekano na ni wazi kabisa kwamba kwa muonekano na hali ya kiafya ya Lowassa ni dhoofu na inazidi kudorora siku hadi siku na kuwakatisha tamaa hata wanaomuunga mkono. Tangu kampeni zianze hakuna mahala ambapo amewahi kuzungumza kwa zaidi ya dakika 15. Hivyo basi, kwa kadiri siku zinavyoenda Watanzania watazidi kubaini kwamba Lowassa hana afya ya kuhimili vishindo vya kampeni wala uwezo wa kumudu majukumu ya Urais. 


7.       Nguvu ya vyama, oganaizesheni na ilani. Magufuli anatokea CCM ambayo kama nilivyoeleza juu ina nguvu ya kuwepo kila kijiji na kila nyumba kumi Tanzania; imetoa marais waliotangulia, na hata wapinzani wametoka katika CCM hiyo hiyo baada ya kukosa nafasi za kugombea kupitia chama hicho. Kwa miaka mitatu iliyopita Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amezunguka kila kona ya nchi akikinadi chama chake, hii ni aina ya kampeni ambayo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Kwa upande wa upinzani hali iko tofauti. Mgombea wao, Lowassa alikuwa mwanachama wa CCM miezi miwili iliyopita, kuingia kwake Chadema kumeleta mpasuko huku Katibu Mkuu wake akitokomea kusikojulikana, na Mwenyekiti wa CUF, Lipumba naye akijiuzulu uongozi kupinga Lowassa kukaribishwa Ukawa. Hii inaonyesha hali si shwari katika upinzani. Kwa sasa Ukawa wanaficha mpasuko huo kwa propaganda lakini madhara yatajitokeza kabla ya siku ya uchaguzi. Moja ya viashiria vya mpasuko katika Ukawa ni kuvunjika kwa makubaliano ya kuweka mgombea mmoja wa Ubunge katika kila jimbo. Zaidi ya asilimia 70 ya majimbo yana wagombea Ubunge toka vyama vyote vinavyounda Ukawa. Kwa mfano Lowassa, kama mgombea Urais wa Ukawa, akienda Ubungo ambapo kuna wagombea toka Chadema, CUF na NCCR atamnadi mgombea yupi?

8.       Kuondoka kwa Dr Slaa Chadema, tuhuma za Mbowe kuiuza Chadema kwa Lowassa kwa TZS bilioni 10 (ambazo Dr Slaa amezithibitisha) na ukawa kuhama kutoka kumuita Edward Lowassa fisadi mkuu wa nchi miaka michache iliyopita hadi sasa kumfanya kuwa mgombea wao. Hii imewakanganya Watanzania wengi na wote wanaochukua muda kulitafakari wanazidi kupata maswali zaidi. Uamuzi wa mpigakura katika hali kama hii ni kuendelea kulipigia kura zimwi alijualo (CCM) kuliko zimwi jipya asiloelewa (Ukawa). 

9.       Matumizi makubwa ya fedha katika kutafuta madaraka. Mpaka mwisho wa mwezi Agosti 2015 Lowassa alikuwa tayari ametumia zaidi ya TZS bilioni 106 kwa kipindi cha miaka miwili na nusu kwanza kutafuta nafasi kugombea ndani ya CCM na kisha kuhamia Ukawa. Wananchi wengi wanahoji zinapotoka fedha hizi, wengi wakikumbuka kauli ya Mwalimu Nyerere kwamba “Mtanzania wa leo hawezi kukununua kabla ya yeye kwanza kununuliwa”. Wananchi wanahoji namna gani Lowassa anapanga kurejesha fedha hizi iwe zake (pia wanahoji kazipataje) au za marafiki zake (lengo lao kumpa fedha ni nini). Magufuli hana kashfa ya namna hii na hata kampeni zake za kuomba kuteuliwa ndani ya CCM  hazikuwa za matumizi ya fedha kabisa. Kama wananchi watapiga kura kwa kuangalia uadilifu katika kupata na kutumia fedha, na pia kama watapiga kura wakiamini kwamba Ikulu si mahali pa kufanya biashara ili mtu arejeshe fedha alizotumia wakati wa kampeni na kuhonga kupata nafasi basi Magufuli ana nafasi kubwa ya kushinda. 

10.   Mzimu wa Mwalimu Nyerere: Mwaka 1995 Mwalimu Nyerere alisema wazi kwamba Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania, alikatwa jina lake kwa haki (video ya Mwalimu akisema haya  iko mitandaoni na ni moja ya video zinazotazamwa kwa wingi wakati huu wa uchaguzi mkuu) na hakuna maana kuendelea kumjadili na kwamba chama kisonge mbele. Watu wanaomjua vizuri Lowassa na shughuli anazozifanya wanasema kwa miaka 20 Lowassa hajabadili zile sifa zilizomfanya Mwalimu kutamka maneno yale mwaka 1995. Hata alipoomba familia ya Mwalimu Nyerere kumuunga mkono alipoondoka CCM alijibiwa wazi kwamba yeye hajawahi kuwa chaguo la Mwalimu.  Watanzania bado wanamuheshimu na kumuamini Mwalimu Nyerere na ni wazi watachagua kiongozi wakifuata wosia wake. Uadilifu wa Magufuli utamuwezesha kuaminiwa na Watanzania na kushinda nafasi hii. 

PICHA UZINDUZI WA KAMPENI JIMBO LA MOROGORO MJINI


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Fikiri Juma akimnadi Mgombea Ubunge Wa Jimbo hilo Mh Aziz Abood wakati wa Uzinduzi wa Kampeni za Jimbo hilo.Ikumbukwe Mh aziz Abood anatetea Kiti cha Ubunge wa Jimbo hilo Mara baada ya Kuongoza Jimbo hilo kwa Miaka 5 Kwa mafanikio ya Hali ya Juu.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini wakiwaasa wakazi wa Jimbo la Morogoro Mjini Kumchagua MH John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini wakiwaasa wakazi wa Jimbo la Morogoro Mjini Kumchagua MH John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Akiwahutubia Mafuriko ya wakazi wa Jimbo la Morogoro Mjini waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Kampeni za  Ubunge za Jimbo hilo




Wakazi wa Jimbo la Morogoro Mjini waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa Kmpeni za Ubenge na Madiwani wa Jimbo hilo

MAGUFULI MKOANI RUVUMA























MAGUFULI AWEKA HISTORIA MAJI MAJI SONGEA


  • Maelfu  wahudhuria mkutano wake wa Kampeni
  • Asema Serikali yake haitoruhusu mkulimwa kukosa
  • Ataboresha maslahi ya walimu
  • Asisitiza Elimu bure kutoka kidato cha kwanza mpaka cha nne


 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Maji Maji tayari kuhutubia,kuomba kura za Urais, Ubunge na Madiwani kwa wananchi wa Songea mjini.
  Vijana wakifurahia ujio wa Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli mjini Songea.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa Songea mjini waliofurika kwenye uwanja wa Maji Majikumsikiliza wakati wa kujinadi kwenye mkutano wa Kampeni za CCM.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa mji wa Songea ambapo alisema katika serikali yake wakulima hawatokopwa mazao yao, mbolea zitapatikana kwa wakati, barabara zitaboreshwa ,elimu bure mpaka kidato cha nne, kuongeza maslahi ya walimu pamoja na kuboresha huduma za afya.

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCm Dk. Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Songea mjini ambapo aliwataka wananchi hao kumpa kura nyingi Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli kwenye uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25.
 Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Ndugu William Lukuvi akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Maji Maji.
 Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Anastaz Mpanju akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye mkutano wa Kampeni za CCM ambao Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli alihutubia . 
 Injinia Stella Manyanya akiwa ameketi pamoja na Wazee wa Mji wa Songea wakati wa mkutano wa kampeni za CCM kwenye uwanja wa Maji Maji.
 Mwigulu Nchemba akihutubia wakazi wa Songea mjini na kutaka wasihadahike na watu wenye uroho wa madara .
 Jamaa kapiga Magufuli staili kwenye mkutano wa kampeni za CCM uwanja wa Maji Maji.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Peramiho mkoani Ruvuma.
 Wakazi wa Peramiho wakifurahia hotuba ya Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli 
 Umati wa wakazi wa Peramiho wakisikiliza hotuba ya Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuliwakati wa mkutano wa kampeni.
 Haya ndio mafiga matatu ya Peramiho.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea ubunge wa Jimbo la Mbinga Ndugu Sixtus Mapunda kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mbinga mjini.
 Mgombea ubunge wa Jimbo la Mbinga mjini Sixtus Mapunda akihutubia mbele ya Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufulikwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika Mbinga.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mbinga.
 Wanachama na Viongozi wa CCM wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni Mbinga.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza wakati
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa Mbinga.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Kigonsera wakati akiwa njiani kuelekea Mbinga mjini.

 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Kapteni John Komba ,Lituhi.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuliakisali mbele ya jkaburi la Kapteni John Komba.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuliakihutubia wakazi wa Lituhi kwenye mkutano wa kampeni ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa serikali itajenga daraja kwenye mto Luhuhu.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mgombea ubunge wa jimbo la Nyasa Injinia Stella Manyanya kitabu cha Ilani ya Uchaguzi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCm uliofanyika Lituhi.
 Mwenyekiti pekee wa Kitongoji kutoka Chadema Ndugu Sixbert almaarufu kama Seaman akitangaza kujiunga na CCM kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufulialifanya kampeni zake.

 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Lituhi.