Saturday, August 29, 2015

UKAWA YA GONGA KISIKI JANGWANI, LOWASSA AIZIKA CHADEMA

Hebu tujikumbushe yalio tokea leo Jangwani na yaliyo semwa na Loassa mgombea wa Ukawa aka Chadema.
1: Lowassa amesema atamtoa Babu Seya akiwa Rais. Je huko sio kuingilia utawala wa sheria? Je ana uhakika gani alisingiziwa? Hivi ndio vipaumbele vya serikali kwenye nchi yenye matatizo kiasi hichi? Tokea lini Lowassa amekua hakimu? Je, na wafungwa wengine atawaachia huru? 
2: Lowasa kasema atatuletea/kumfufua Balali, sasa najiuliza si watuambie leo hii yuko mji gani ama nchi gani na kwanini asubiri awe raisi ndio watuletee Balali? Hichi nacho ni kiapumbele? Au hii ndio ilani ya UKAWA?
3: Lowasa kasema eti, elimu itakuwa bure! Kuanzia primary-University lakini ameshindwa vibaya sana kusema fedha zitatoka wapi? Hivi, wakati wa Nyerere nani alilipia elimu? 
4. UKAWA wamekiri wao ni ma lofa kutokana na t-shirt walizotengeneza na kuuza uwanjani lakini hapo hapo wameambiwa wakasome hotuba ya mgombea Urais mtandaoni je kama ni kweli ni ma lofa wana access ya internet? Kulikuwa kuna aja gani ya mkutano kama mngeweka vitu vyote online? Vipi kuhusu wazee wa Mashambani, nao waingine dot com kusoma ilani?
5. Ukawa wametuhakikishia kuwa hawana sera wala ilani zaidi ya kufukuza upepo.
6. Ukawa wamebakia kumjibu Mtaafu Rais Mkapa ambaye aliwateka Kisaikologia na kuwa gumza la Ukwa leo Jangwani.

No comments:

Post a Comment