Thursday, October 29, 2015

MATOKEO MATOKEO MATOKEO TANZANIA

Saa Tisa na Dakika Hamsini Tarehe 29/10/2015 Jaji wa Rufaa (Mst.) Damiani Z. Lubuva MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI amesaini Matokeo na amemtangaza Dkt. John Pombe Magufuli Kuwa Mshindi wa Urais Katika Uchaguzi Mkuu 2015.
Ametoa Takwimu za Majumuisho ya kura kama ifuatavyo;
Dkt. John Pombe Magufuli (CCM) ana jumla ya Kura 8,882,935 (58.46%)
Mh. Lowassa (CHADEMA) ana jumla ya kura 6,072,848 (39.97%)
Hivyo Basi Dkt. John Pombe Magufuli ameongoza na kuibuka mshindi kwa Jumla Ya Kura 2,810,087 (Millioni Mbili Laki Nane Elfu Kumi na Themanini na Saba) dhidi ya Mh. Lowassa na wagombea wengine.
VIVA MAGUFULI VIVA WATANZANIA
‪#‎TanzaniaKwanza‬
‪#‎AmaniKwanza‬

No comments:

Post a Comment