Saturday, October 31, 2015

NI NDOTO ZA MCHANA KUDHANI KUWA CHADEMA ITASHINDA KESI YA UCHAGUZI HUKO ICJ.



Kuna mahali huku kwenye mitandao ya kijamii ambapo nimeona "Makamanda" wakitoa taarifa kwa wanachama, mashabiki, na wapenzi wa UKAWA kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA Ngazi ya Taifa Bw. Freeman Mbowe na Mhe. Edward Lowassa wamekwenda Kufungua mashtaka kwenye mahakama ya kitamataifa ya ICJ na kwamba wadau wa UKAWA wawe wapole kwani mafanikio yatapatikana. 
Mafanikio yanayotegemewa hapo ni kwa CHADEMA kushinda Kesi na hivyo kutolewa kwa hukumu ambayo 'itawabeba' CHADEMA.
Bila ya kupotezeana muda na kupeana matumaini hayo ya UKAWA yasiyo na kichwa wala miguu ni kwamba, hapo hakuna kesi kwa sababu;-
1. Kwanza kabisa Mahakama ya ICJ HAINA Mamlaka ya kushughulika na kesi zilizopo kwenye mfumo wa sheria za ndani na Katiba za Nchi wanachama kwa sababu kubatilisha Katiba ya Nchi au Sheria zitokanazo na Katiba ya Nchi Mwanachama ni kuingilia Mamlaka ya Nchi husika na ilhali mamlaka ya nchi inapaswa kulindwa na kuheshimiwa bila ya kuingiliwa na Mtu yeyote au taasisi yoyote. Mamlaka ninayoizungumzia hapa ni "Sovereignty" na siyo vinginevyo. Kazi za Mahakama ya ICJ ni
(a) Kwanza, Kushughulikia kesi za kimataifa zinazohusu Nchi wanachama. Kwa maana hiyo Nchi ndiye mshtaki au mshtakiwa na sio vinginevyo. Mf. wa Mashauri ya staili hiyo ni i.e Mgogoro wa Mpaka kati ya Malawi na Tanzania.
(b) Pili, Kushughulikia kesi za taasisi za jumuiya za kimataifa hizi taasisi kwa lugha ya kiingereza tunaziita "Public International Organizations" kwa maana ya kwamba uwepo wa hizi taasisi unatokana na makubaliano ya Nchi mbili au zaidi katika kuanzisha jumuiya. Mf. wa taasisi ni Shirika la Afya Duniani (WHO) Shirika la UKIMWI (UNAIDS) n.k Mfano wa hizi jumuiya za kimataifa ni
(i) Jumuiya zinazotokana na miktadha ya kijiografia yaani "Geopolitical Intergovernmental Organizations" Mfano; Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Jangwa la Sahara (South African Development Community = SADC) Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (International Conference on Great Lakes Region = ICGLR) Jumuiya ya Afrika Mashariki (East African Community = EAC) n.k
(ii) Jumuiya zinazotakana na makubaliano ya kimataifa kwa maana ya Bilateral and Multilateral Relations) hapa tuna Jumuiya kama vile Umoja wa Mataifa (United Nations = UN) na nyinginezo
Sasa hizi jumuiya huanzisha taasisi zake ambazo malengo ya hizo taasisi ni kufanikisha uetekezaji wa shughuli na kufikia malengo makuu ya jumuiya husika ambapo taasisi anzishwa zimeasisiwa kwazo.
Kwa Mantiki hiyo sasa jumiya hizi na taasisi zake ndio hufungua mashauri kuko ICJ na siyo taasisi za ndani ya nchi kwa maana ya "Local Institutions"
(c) Tatu, ICJ hushulikia kesi za taasisi binafsi za kimataifa yaani (Private International Organizations) Taasisi binafsi za kimataifa ni zile taasisi ambazo usajili wake umetokana na sheria za nchi A lakini taasisi hiyo inafanya kazi katika Nchi B sasa taasisi inapotoka katika Nchi A na kwenda kufanya kazi katika Nchi B huko Nchi B hiyo taasisi itafahamika kama taasisi binafsi ya kimataifa kwa maana ya kwamba inafanya kazi katika nchi ambapo usajili wake hautokani na sheria za nchi hiyo. Haya huwa ni makampuni au mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Mf. Richmond mliyoambiwa n.k
Sasa ikitokea kwamba ile taasisi ya kigeni iliyosajiliwa kama taasisi ya kimataifa kule Nchi B lakini asili yake ni Nchi A na kwamba katika kufanya kwake kazi huko Nchi B iliwahi kushtaki au kushtakiwa kwa mujibu wa sheria za Nchi B lakini wakati yenyewe inatokana na sheria za Nchi A na haikuridhika na hukumu iliyotolewa kwa mujibu wa Nchi B sasa inaweza kwenda ICJ ili kuomba mapitio ya hukumu (Judgement review), au kukata rufaa (Appeal) kwa sababu haijaridhika na hukumu za sheria za Nchi B kutokana na yenyewe kuasisiwa katika mfumo wa sheria za Nchi A kwa hiyo hapo sasa ICJ wanasikiliza shauri husika na kulitolea maamuzi.

Mpaka hapo hakuna nafasi ya CHADEMA kusikilizwa huko ICJ.
Pia kesi za Richmond na kesi nyingine zinazofanana na hizo za kesi ya Richmond hazihusiani kabisa na kesi ya Uchaguzi hasa kwa aina ya Uchaguzi huu wa Mwaka 2015.
2. Kama ni kweli kuwa CHADEMA wameishtaki CCM hapo tena hamna kesi kwa sababu kitaalamu katika fani ya sheria wahusika (parties) katika shauri lazima wahusiane kisheria ( Appellant vs Respondent or Plaintiff vs Defendant or Applicant vs Respondent)
katika shauri la CHADEMA dhidi ya Uchaguzi CHADEMA wanapaswa kuwashtaki Tume ya Taifa ya Uchaguzi CCM inaweza kutajwa kwenye shauri kama mjimbu mashtaka Na. 2 maana CCM ni "third party" sasa kama CCM ni mshtakiwa Na. 01 na NEC kama Mshtakiwa Na. 2 kitu ambacho kama ndivyo ilivyo basi wamechemka. Sababu za wao kuchemka ni kuwa;-
(a) Mwenye mamlaka ya kuendesha uchaguzi katika hatua zote ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi na SIYO CCM. Hii ni kwa mujibu wa Ibara ya (74) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, Sheria ya Uchaguzi ya 1985 na kanuni zinazotokana na sheria ya Uchaguzi. CCM yeye ni mshiriki katika Uchaguzi kama alivyo CHADEMA na CCM haiwezi kupeleka vielelezo ICJ kwa sababu yenyewe siyo Mamlaka iliyotangaza Matokeo. Yaani swali la kisheria hapa ni kuwa "Kwa nini Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 katika Ngazi ya Urais yasibatilishwe?" sasa hapa utahusisha Ibara ya (41) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inayozungumzia Utaratibu wa Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Kwa mantiki hiyo swali tajwa hapo juu linatajiwa na tume na SIYO CCM.
Pia, Mgombea hawezi kujitangaza kuwa kashinda kwa vielelezo alivyo navyo hata siku moja kwa sababu ni vigumu kuthibitisha uhalali wa vielelezo anavyovitumia Mgombea husika katika kujitanabaisha kuwa ameshinda Uchaguzi. Lakini Tume ndiyo mamlaka halali ya kisheria ambayo inaweza kuthibitisha uhalali wa matokeo iliyotangaza na majaji huwa na utaratibu wa kutathmini (assessment) ushahidi uliowasilishwa kaba ya kutumia ushahidi huo kuwa uthibitisho ( Evidence to Exhibit Process)
sasa kwa hali hiyo ni kwa vipi CHADEMA inaweza kuthibitisha uhalali wa vielelezo vyake kuwa ilishinda uchaguzi mkuu wa Urais wa mwaka 2015??? na kila mgombea akiibuka na nyaraka zake yupi ataonekana mkweli maana "kura ni siri".
Mpaka hapo wana CCM kuweni wapole Rais ni Magufuli na hawa mabwana watatapa mwisho watashindwa.
Hata Raila Odinga wa Kenya aliposhindwa Uchaguzi Mkuu wa Kenya mnamo Mwaka 2013 walienda Mahakani wakalalamika wakasikilizwa wakashindwa na baadae Kenyatta akaapishwa. Hata hapa Tanzania itakuwa hivyo hivyo.
RAI YANGU
UKAWA hawakuanzia mbali kwa hiyo wasingeweza kufika mbali
‪#‎UKAWA_WAKAJIPANGE_UPYA‬
MAREJELEO
1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 (Ibara ya 41, na 74).
2. Sheria ya Uchaguzi ya Na. 01 ya Mwaka 1985.
3. Sheria ya taasisi za umma za Kimataifa (Public International Law).
4. Sheria ya taasisi binafsi za Kimataifa (Private International Law).
5. Mkataba wa Umoja wa Mataifa (Charter of United Nations) Sura ya (19), Ibara ya 92 hadi 96).

No comments:

Post a Comment