Friday, November 27, 2015

WAZIRI MKUU MHE KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI.

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta madudu.
Maafisa hao, ambao majina yao yamehifadhiwa (kwa sasa) ili Jeshi la Polisi liweze kuwashughulikia, wametakiwa pia kusalimisha hati zao za usafiri.
Imegundulika kwamba kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo data za Mamlaka ya Bandari inazo lakini katika mtandao wa TRA hayaonekani ‪#‎SasaKaziTu‬



No comments:

Post a Comment