Wednesday, November 18, 2015

Dkt.Abel Minani, Dkt.John P.J Magufuli na Dkt.John Kyaruzi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam muhula wa mwaka 1985/1986


Wakati mwingine maisha ni kitendawili kikubwa ambacho kinakufanya usijue wewe utakuwa nani kesho! Kesho unaweza kuwa chochote ili mradi unaendelea kuishi. 

Si kila kesho inakuwa na mafanikio au furaha. Kesho nyingine ni chungu na ina maumivu makubwa mpaka kufikia kusema hivi ni kwanini umeumbwa wakati unaishi maisha yasiokuwa na furaha na yenye mateso!? 

Lakini kama ikitokea kesho yako kuwa na furaha, ni rahisi mwanadamu wa kawaida ambaye hafikirii vizuri kujiona kama yeye ndio kila kitu katika duniani na kusahau kuwa ipo siku atakuwa chochote tofauti na alivyo sasa pale mungu anapoamua kumfanya tofauti na alivyo.

Sidhani kama mtu alivyo sasa alitegemea kuwa atakuwa hivyo! Ebu fuatilia hii picha kisha ujiulize muheshimu rais wetu alijua kuwa atakuwa alivyo sasa?!

Mungu kamsaidia kesho yake inaishia kwa furaha ingawa ina changamoto nyingi. Mungu ambariki sana.

Kutoka Kushoto: Dkt.Abel Minani, Dkt.John P.J Magufuli na Dkt.John Kyaruzi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam muhula wa mwaka 1985/1986.

No comments:

Post a Comment