Friday, November 20, 2015

"UKAWA" Watawezaje kuwawakilisha wananchi katika majimbo yao kwa staili hii?



Bado najaribu kufikiria hawa ukawa nini hasa dhamira yao ya kufanya fujo na hatimae kufukuzwa kutoka ndani ya ukumbi wa bunge!

Watawezaje kuwawakilisha wananchi katika majimbo yao kwa staili hii?! Mi nafikiri busara itumike ili waweze kutumikia majimbo yao.

vinginevyo wanapoelekea upinzani na ukawa havitakuwepo katika siasa kwa sababu watampa nafasi mpinzani wao mkubwa ambae ni ccm kwa kufanyakazi zake kwa nafasi huku wakijipanga kuutokomeza upinzani.

Tunaomba mtumie njia nyingine ili mpate kutusaidia sisi wananchi vizuri kuliko kufanya fujo na mwishowe kufukuzwa bungeni.

Swali langu ni:- watarudi tena bungeni januari au ndio basi tena?!

No comments:

Post a Comment