Wednesday, December 9, 2015

Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu akifanya usafi kuunga agizo la Rais Magufuli



Makamu wa Rais wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hasssani amewataka watanzania kuunga mkono hatu za serikali inazochukua kwa kuwa inadhamira ya dhati ikiwa sambamba na tukio muhimu la leo la siku ya sherehe za Uhuru ambalo limetumika kuweka mazingira safi kuepuka magonjwa ya Mlipuko.

Akiwa Eneo la OSTERBAY jijini Dar es Salaam wakati akiungana na wananchi kufanya usafi ameweza kuyasema hayo ambapo wananchi waliokuwepo eneo hilo kufanya usafi wanasema kuwa kujitokeza huko kwa viongozi kuungana nao kufanya usafi wanaendelea kuwa na matumaini na serikali ya Awamu ya Tano kuwa inadhamira kubwa ya dhati kuhakikisha afya za watanzania zinaimarika kwa mazingira kuwa safi.


Na Mr. Chin

No comments:

Post a Comment