Waziri mmoja nchini Kenya amejipata taabani baada ya uchunguzi kugundua kuwa wizara yake ilinunua kalamu moja kwa dola 100.
Waziri wa ugatuzi bi Ann Waiguru, anatakiwa kufika mbele ya kamati ya bunge kuelezea ilikuwa vipi akatumia kiwango hicho cha fesha za umma.
Mbali na kalamu iliyogharimu dola 100, bi Waiguru pia alinunua runinga ya afisi yake kwa gharama ya dola $19,000,
Kipakatilishi (Laptop) kwa gharama ya dola $11,000 zulia ya afisi yake kwa gharama ya dola $ 3,800 programu ya kulinda kompyuta isiambukizwe virusi kapersky kwa gharama ya dola 9,737.
Programu ya Adobe kwa gharama ya $19,000.
Kifaa cha kutoa kondomu kiligharimu wiazara hiyo ya Ugatuzi dola $250 kila moja.
Waziri huyo sasa amesema kuwa hizo zote ni njama za kumpaka tope kwani yeye mwenyewe hana doa na kuwa ataendelea kuhudumia taifa kwa mujibu wa wajibu aliopewa na rais Kenyatta.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari, Waziri waiguru anasema kuwa, yeye siye anayenunulia wizara hiyo bidhaa kwani hilo ni wajibu wa afisa anayesimamia ununuzi wa bidhaa na huduma katika wizara yake.
Bi waiguru anakanusha kuwa anamiliki runinga ya gharama hiyo katika afisi yake.
Hii si mara ya kwanza kwa bi Waiguru kuhusishwa na ubadhirifu mkubwa wa mali ya umma na Ufisadi.
Takriban mwezi mmoja uliopita, Waiguru alitajwa katika sakata ya malipo katika idara ya huduma kwa vijana ya taifa NYS.
Yamkini NYS ilipoteza takriban dola milioni nane $ 8,000,000 kupitia kwa malipo ghushi kwa wanakadarasi wachache waliokuwa na uhusiano na maafisa wa ngazi za juu katika wizara.
Source BBC
No comments:
Post a Comment