Saturday, November 14, 2015

UCHAGUZI MKUU ZANZIBAR KURUDIWA.

“Mimi Jecha Salim Jecha, mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 119 (10) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na kwa mujibu wa vifungu vya 391) na 5 (a) vya Sheria ya Uchaguzi namba 11 ya mwaka 1984, natangaza uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kufuta matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa tarehe 25, Oktoba,”

Tangazo Rasmi la kufutwa kwa matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar katika Gazeti la Serikali la Novemba 6 mwaka huu. Tangazo hilo limetiwa saini na mwenyekiti huyo wa ZEC, Oktoba 28 mwaka huu na kwa msingi huo wananchi wa Zanzibar watatakiwa kuingia tena katika uchaguzi ndani ya siku 90.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, uamuzi huo umechapwa chini ya kifungu Namba 119 (10) na Sheria ya Uchaguzi Namba 11 ya 1984.

Gazeti hilo pia limetolewa kwa kuzingatia kifungu cha 3(1) na 5(a) vya Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar na kuelezea kuwa matokeo yote ya Uchaguzi Mkuu yamefutwa kuanzia Oktoba 25.

Kifungu cha 3 (1) cha Sheria ya Uchaguzi kinasema: “Kanuni, maelezo na matangazo yote ambayo Tume ina mamlaka ya kutunga au kutoa, itajaliwa kuwa yametungwa au yametolewa kisheria kama yametiwa sahihi na mwenyekiti wa Tume au Mkurugenzi wa Uchaguzi.”
©Mwananchi.

No comments:

Post a Comment