Monday, November 16, 2015
JEANNETE KAGAME NI NANI?
Wapendwa wetu, leo tunajibu swali letu liloho.."First Lady yupi unahisi alistahili kuwemo katika listi ya kumi bora kwa mwaka 2015 ambae hakuingizwa?"
Hakuingizwa katika tathmini za mitandao ya kijamii, kisha tukasema watakaoandikwa mara kwa mara tutawaleta na kuwachambua kwa uchache.
Na haya ndio majina yaliyojitokeza mara nyingi zaidi...
1 Janeth Magufuli
2 Regina Lowassa
3 Janeth Kagame (Rwanda)
1 - Janeth Magufuli ni mke wa rais wa Tanzania (First Lady of Tanzania), amekuwa mama wa taifa baada ya kuapishwa kwa mumewe John Magufuli kuwa raisi rasmi wa Tanzania siku ya tarehe 5-11-2015
2 - Regina Lowassa, Katika orodha ya wake wa marais wa Afrika (First Ladies in Africa) jina halimo kabisa. Kwa hiyo hafahamiki katika suali tuloliuliza.
3 - Janeth Kagame, huyu jina lake linaandikwa Jeannette Kagame. Ni mke wa raisi wa Rwanda, Paul Kagame. Huyu ndie chaguo lilostahili kati ya hayo majina matatu yaliyojitokeza kwa wingi kuendana na wakati husika uliyotajwa.
-
Anaitwa Jeanette Nyiramongi Kagame,Amezaliwa 10-8-1962 (10th, August 1962) huko Burundi.
Dini yake ni mkiristu dhehebu la katoliki.
Mwaka 2000, Machi 24 alikabidhiwa kiti cha mama wa taifa (First Lady) baada ya mumewe Paul Kagame kutangazwa kuwa rais rasmi wa Rwanda.
Jeannette Kagame alianzisha IMBUTO FOUNDATION na yeye kuwa ni mwenyekiti, Foundation hiyo inatoa maendeleo ya elimu inayohusiana na masuala ya afya.
Mama Jeannette Kagame pia ni mwanzilishi wa chama kinachokinga na kudhibiti Ukimwi katika familia za kiafrika (PACFA - Protection and Care of Families against HIV/AIDS). Chama hicho chenye malengo ya kuwaandaa watoto juu ya kujikinga na maradhi ya ukimwi kiliitishwa mwezi wa tano mwaka 2001 (May, 2001) mjini Kigali, Rwanda. Baadhi ya wake wa maraisi wa Afrika (First African Ladies) walikuwa wenyeji wa mkutano huo wa kuanzisha PACFA.
Jeannette Nyiramongi Kagame na mumewe Paul Kagame wamebahatika kupata watoto wanne. Watatu wanaume ambao ni Ivan, Brian na Ian. Na mtoto wa kike pekee ni Ange Paul Kagame.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment