Rais Dk. Magufuli akitokea katika ofisi ya Mkurugenzi wa MOI.
Wananchi wakiwemo wauguzi wakishangilia ujio wa Rais Dk. Magufuli katika Hospitali ya Taifa Muhimbili leo.
Rais Magufuli akipata maelezo ya mgonjwa katika wodi ya Sewahaji.
…Akimpa pole bibi aliyelazwa katika wodi ya Sewahaji.
…Akimpa pole mama huyu aliyelazwa katika wodi ya Mwaisela.
…Akizidi kuwapa pole wagonjwa.
Wananchi wakimpungia mkono Rais Magufuli.
Rais Magufuli akimsikiliza mmoja wa wauguzi.
Ulinzi ukiwa umeimarishwa.
Wananchi wakiwa na furaha baada ya ujio wa Rais Magifuli.
Msafara wa Rais Magufuli ukiondoka Muhimbili.
Wananchi wakisindikiza msafara wa Rais Magufuli.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli leo amefanya ziara nyingine ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kujionea hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa.Ujio huo wa ghafla umewafurahisha mamia ya wagonjwa na wafanyakazi wa hospitali hiyo pamoja na wale wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) walioanza kuimba “hapa kazi tu”.
Mmoja wa wagonjwa kutoka MOI aliyejitambulisha kwa jina la Chacha amesema wamepata faraja kubwa baada ya kumuona kiongozi huyo akifika hospitalini hapo.
“Tunampongeza na tunamuombea kila heri katika utendaji wake wa kazi maana ndani ya hospitali hii kuna kero nyingi zinazowakabili wagonjwa waliolazwa wodini,” alisema Chacha.
Rais Magufuli amesema ziara hiyo haikuwa rasmi lakini amejionea kila kitu alipotembea wodi za Mwaisela, Sewa Haji huku akijitahidi kusalimiana na kila mgonjwa.
Awali Rais Magufuli alifika katika Hospitali ya Agha Khan kumjulia hali Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dk. Hellen Kijo Bisimba anayepatiwa matibabu na vipimo katika hospitali hiyo baada ya jana kupata ajali katika makutano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment