Thursday, October 8, 2015

TWENDE NA DK.MAGUFULI KWA MABADILIKO YALIYO BORA NA KWELI


- Ni muumini sana wa umoja,amani na mshikamano. Wakati  wa kampeni zake amekuwa akiwakumbusha na kuwaasa watanzania juu ya umuhimu wa kuitunza amani yetu na kuepukana na siasa za kibaguzi kama udini,ukanda,ukabila au tofauti za kiitikadi kwani maendeleo ya kweli hayana ubaguzi na hayawezi kupatikana kama vitu hivyo havipo.
-Amesema elimu bora ni chachu ya ujenzi wa uchumi wa kisasa hivyo mbali na kuifanya elimu kuwa bure kuanzia msingi hadi kidato cha nne serikali itahakikisha inawekeza zaidi katika kuwapatia watanzania elimu bora na ya kisasa ili waweze kumudu changamozo zilizopo pamoja na ushindani katika dunia ya kileo.
- Ni mkweli,muadilifu na anafahamika kwa uchapakazi,ufuatiliaji.na misimamo isiyombishwa katika kuzisimamia sheria,taratibu na kanuni. Amekuwa mara zote akisisitiza kuwa hawezi kusema uongo kwa sababu anataka kura bali kama kiongozi anao wajibu wa kuwaeleza ukweli kwani msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

- Pia,amekuwa akisisitiza wapo baadhi ya watendaji na viongozi wa serikali wana tabia za uzembe,rushwa,ufisadi,wizi na ubadhirifu katika kuwatumikia watanzania, ambapo aliwaahidi watanzania kuwa wanamfahamu kwa utumishi wake akiwa katika wizara mbalimbali hivyo MAGUFULI yule bado hajabadilika na anamuomba Mungu na kututaka nasi kumuombea asibadilike kwani hawa atakula nao sahani moja katika kuhakikishaa watanzania wanapata maendeleo ya kweli.Hapa akasisitiza maadam hakutumia hata senti moja kuhonga ili ateuliwe basi sadaka yake kwa watanzania ni utumishi uliotukuka.
- Ni muumini wa falsafa ya kujikosoa na kukosolewa kwani amekuwa mara zote akikiri kuwa mbali na kazi kubwa zilizofanywa na marais waliopita lakini yapo maeneo hayakufanywa vizuri hivyo atahakikisha anayaenzi yale mema na kuboresha yale ambayo yanaonekana kuwa kero au changamoto bado kwa wananchi katika kuona wanapata huduma bora na wanajiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
- Ameahidi kuwa serikali yake itawajali watumishi wa serikali kwa kuwapa mishahara mizuri ila amewaomba nao wasimuangushe wachape kazi kwelikweli kwani atakuwa mkali sana kwa wazembe. Pamoja na kuhakikisha wafanyakazi wa sekta binafsi wakiwemo madereva,wahudumu wa mahotel,wafanyakazi wa ndani n.k wanapewa mikataba inayoeleza mishahara,posho,bima ya afya n.k ili wanufaike na kutokunyanyasika. Hapa pia ameahidi serikali yake itahimiza ujenzi wa miundombinu ya kibiashara kwa wamachinga,mama ntile na bodaboda huku akisisitiza hawatanyanyasika kamwe.
- Dk. MAGUFULI mbali na kukiri ajira ni tatizo kubwa ameeleza hatutaweza kupunguza tatizo hili pasipo kuhimiza kilimo cha kisasa na ujenzi wa viwanda ndiyo maana ilani anayoinadi ya CCM imesisitiza Tanzania ya viwanda ifikapo 2020. Ambapo amekuwa akisisitiza katika kufanikisha uchumi wa viwanda serikali itashirikiana na sekta binafsi ili kufanikisha malengo haya. Hapa amesisitiza serikali yake itaweka mazingira rafiki ili kuwaondolea urasimu na vikwazo wote watakaokuwa na lengo jema la kuwekeza katika viwanda. Amesisitiza serikali itajenga viwanda bila kutegemea fedha za wahisani bali kwa kutumia vizuri mapato yetu na rasilimali tulizo nazo.
- Ameahidi kuwafikishia umeme 60% ya watanzania waishio vijijini ifikapo 2020 ili uwe chachu kwao kufikia maendeleo bora zaidi. Hapa akawahakikishia kuwa serikali yake itapunguza kodi katika vifaa vya ujenzi ili wananchi wamudu gharama za ujenzi na hivyo kuiliki nyumba bora za makazi na hata biashara.
- Dk. MAGUFULI amesema ni ukweli uliyo wazi kuwa ili kujitegemea kibajeti ndiyo siri pekee katika kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi. Ambapo ameahidi kuongeza makusanyo ya kodi na kuona wananchi wengi zaidi wanaopaswa kulipa kodi wanafanya hivyo kwa kutazama viwango wanavyotozwa ili wawe wanavimudu, kusimamia vizuri matumizi ya mapato ya serikali ili wananchi wanufaike nayo kupitia miradi ya maendeleo. Huku akisisitiza kufuta misamaha ya kodi isiyo na tija pamoja na usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato yatokanayo na madini,utalii,uvuvi na misitu.
-Katika kuifungua zaidi Tanzania kiuchumi serikali yake itajenga reli mpya ya kisasa "Standard gauge" kwa kushirikiana na sekta binafsi. Katika ilani ya CCM ukurasa wa 53&54 inazitaja njia za reli zifuatazo ndiyo zitajengwa: Dar-Tabora-Mwanza/Kigoma; Uvinza,Msongati(Burundi); Isaka-Kigali(Rwanda); Mtwara-Songea-Mbambabay(Na Matawi ya kwenda Mchuchuma na Liganga); Tanga-Arusha-Musoma; & Kaliua-Mpanda-Karema. Kujenga viwanja vipya vya ndege na kukarabati baadhi.
- Dk. MAGUFULI pia ameahidi Kuhakikisha mawasiliano ya simu za mkononi yanawafikia wananchi wote Tanzania Bara na Zanzibar, kuimarisha miundombinu ya TEHAMA ili kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii na kiuchumi kwa wananchi walio wengi zaidi pamoja na kuwalinda watumiaji wa simu za viganjani dhidi ya dhuluma,wizi na uhalifu wa mitandao.
- Dk. MAGUFULI pia amesema Serikali ya awamu ya nne imefanya vizuri sana katika kuwafikishia maji safi na salama watanzania waliowengi yeye atahakikisha anawafikishia watanzania wote waliobaki ili kuwaepusha na magonjwa na kuwapa muda wa kushiriki shughuli za uzalishaji badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji safi na salama.
-Ameahidi kuwa serikali yake itakuwa ya kazi tu. Na ndiyo maana ataunda baraza la mawaziri lililo dogo, lililojaa waadilifu na wachapakazi ili kuwatumikia watanzania kwa masaa 24 katika kuipaisha Tanzania kimaendeleo. Hakika haya ndiyo mabadiliko yaliyo bora na kweli.
KURA YANGU,YAKO NA YULE AIPATE OKTOBA 25, 2015

No comments:

Post a Comment