Saturday, October 31, 2015

Nyumbu ni mnyama mwenye akili ndogo kuliko wote




NYUMBU ni wanyama wa ajabu, nadhani ni wanyama walio na akili ndogo kuliko wanyama wote wa porini. Wanyama hao wakishaamua kufanya kitu watakifanya tu bila kujali ni madhara gani yatatokana na uamuzi wao.

Mfano Nyumbu wanaweza kuwa na kiu wakaamua kwenda kunywa maji kwenye mto uliojaa mamba. Kwa wingi wao watafika mtoni na kuanza kunywa maji huku mamba wenye njaa kali wakijikamatia nyumbu mmoja mmoja wakizamisha majini na kujitafunia. Nyumbu waliobaki wataendelea kunywa maji bila kujali yanayowakuta wenzao, wakimaliza kunywa maji wanaondoka zao, lakini wakisikia kiu tena wanarudi palepale bila kukumbuka kuwa kuna wenzao waliotafunwa, na wanaendelea kutafunwa wengine!

Au wakati mwingine Nyumbu wanaweza wakaamua kuvuka mto wenye kina kirefu, kwa kuutegemea wingi wao, wataingia kwenye mto ambapo karibu nusu yao watabaki maiti katika mto huo wenye kina kirefu huku wengine wakifanikiwa kuvuka.

Daima hayo ndiyo maisha ya Nyumbu, kukilenga ili wakitimize kile wanachokiangalia kwa wakati huo bila kujali madhara ya baadaye.

Tofauti na Nyumbu binadamu tumejaliwa akili, pamoja na matatizo na shida tunavyoweza kuwa navyo, katika kuvikabili ni lazima tupime madhara na faida ya kufanya hivyo. Kama madhara yanazidi faida tunaona bora tuache. Ni heri mtu kubaki na shida au matatizo kuliko kutoa uhai kwa tamaa ya kutaka kumaliza matatizo au shida.


Je, Watanzania tunakubali kugeuzwa Nyumbu?

No comments:

Post a Comment