Sunday, October 25, 2015

KURA YA MAAMUZI KUHUSU KATIBA YAANDALIWA CONGO

Sassou Nguesso
Sassou Nguesso ni miongoni mwa marais walioongoza muda mrefu zaidi Afrika
Congo-Brazzaville inaandaa kura ya maamuzi leo kuhusu marekebisho ya katiba ambayo yatamuwezesha Rais Denis Sassou Nguesso kuwania kwa muhula wa tatu.
Viongozi wa upinzani wamewataka watu kususia kura hiyo baada ya waandamanaji kadha kufariki kwenye makabiliano na maafisa wa usalama.
Chini ya katiba ya sasa, rais huyo hawezi kuwania tena kwa sababu amepitisha umri wa miaka 71 na pia amehudumu mihula miwili tayari.
Rais Sassou Nguesso aliingia mamlakani mara ya kwanza mwaka 1979.
Kwa sasa anamalizika muhula wa pili wa miaka saba. Alishinda uchaguzi mkuu wa majuzi zaidi 2009 kwa karibu asilimia 79. Uchaguzi huo ulisusiwa na nusu ya wagombea wa upinzani.
Maelfu ya watu walishiriki maandamano ya Amani dhidi ya utawala wa Sassou Ngueso Septemba.
Mnamo Jumanne, maafisa wa usalama walipotawanya wa nguvu waandamanaji mji mkuu wa Brazzaville na mji mkubwa kiuchumi wa Pointe-Noire, watu wane walifariki.
Waandamanaji waliambia BBC kuwa maafisa wa usalama walitumia risasi halisi na kwamba helikopta za jeshi zilitumiwa. Wanaharakati kadha na viongozi wa upinzani wamedai kutishwa na maafisa wa serikali.
Matokeo ya kura hiyo ya Jumapili na jinsi raia wa Congo watayapokea, vitafuatiliwa kwa karibu katika mataifa yaliyo karibu.
Marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda pia wanatarajiwa kujaribu kuwania kwa mihula ya tatu, mwandishi wa BBC Maud Jullien anasema.
Rais Sassou Nguesso ni miongoni mwa viongozi wa sasa Afrika waliokaa madarakani muda mrefu zaidi.BBC

No comments:

Post a Comment