Wednesday, October 14, 2015

MWIGULU NCHEMBA SASA ATUA KANDA YA ZIWA,AMUOMBEA KURA MAGUFULI MAJIMBO 6

Mwigulu Nchemba Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi akimnadi Mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Busega Dr.Chegeni mapema hii leo.Mwigulu Nchemba Jimbo la Busega kwa Dr.Chegeni akisisitiza Wananchi kwenda kupiga kura kwa wingi,Hakuna namna CCM itashinda kwa kishindo kama wananchi hawajitokezi kupiga kura,Kura ni kwaajili ya maamuzi makubwa ya Taifa lako.Wananchi wa Sumve wakionesha Umoja wao kwenye zoezi la kwenda Kuichagua CCM kwa nafasi zote.Mwigulu Nchemba akimnadi Mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Sumve Nd.Ndasa.Mwigulu Nchemba akiondoka Jimbo la Sumve mara baada ya kuomba kura za Urais,Ubunge na Udiwani kwa Chama cha Mapinduzi.Mwigulu Nchemba akiwasisitiza Wananchi wasipuuzie jambola kupiga kura,Pia ameonya wananchi wanaouza vitambulisho vya Kupigia kura kuwa ni kosa la kisheria na Kila mmoja anapaswa kutunza kitambulisho chake.Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndg.Anton Diallo,Mwigulu NChemba na Mh.Charles Kitwanga .Mbunge wa Jimbo la Misungwi Ndg.Charles Kitwanga akizungumza na Wananchi wake kuwa ameshajipanga kuhakikisha  Miradi yote aliyoiianzisha anaikamilisha kwa miaka 5 ijayo.Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Solwa hii leo.Mwigulu Chemba akisalimiana na Mgombea Ubunge Jimbo la Solwa ndg.Salum.Mwigulu Nchemba akiteta Jambo na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Bi.Azza Hilaly.Comrade Mwigulu Nchemba akiagana  na Wananchi wa Jimbo la Solwa.Hisia za Mwananchi kwa Rais mtarajiwa Dr.J.Pombe Magufuli.Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa shinyanga hii leo "Nawaasa wananchi wa shinyanga Mjini,Muacheni Masele aendelee kusimamia malengo yake,ameshaonesha uwezo wa kusimamia shughuli za maendeleo Jimboni na serikalini.Hakuna haja ya kubadilisha Mbunge wakati hivi sasa ndio Vijana wanaotegemewa kusimamia Serikali hii ya CCM inayokuja.Ubunge sio Fashion kwamba kila siku unaweza kubadilisha"Mwigulu.CCM "Chama kipo Imara"Wananchi wakishangilia moja ya sentensi za Mwigulu Nchemba "Mgombea wa CCM anauwezo wa Kusimamia jambo na likafanikiwa,ameonesha uwezo huo akiwa waziri nasasatumpatie asimamie Wizara zote".Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndg.Anton Diallo akimnadi Mbunge mtarajiwa kwa awamu ya pili Shinyanga Mjini Ndg.Steven Masele.Wananchi wa wakifuatilia Mkutano wa kampeni wa Chama Cha Mapinduzi hii leo Shinyanga Mjini.Mbunge mtarajiwa wa Chama cha Mapinduzi Shinyanga Mjini Ndg.Steven Masele akizungumza na Wananchi wake,Ameahidi kuendelea kusimamia ujenzi wa Viwanda mbalimbali ndani ya Wilaya ya Shinyanga Mjini ambapo hadi sasa viwanda vitano vimeshajendwa kati ya 12 vinavyotakiwa Kujengwa kwa Shinyanga.Mwigulu Nchemba akiagana na Viongozi na Wananchi wa Shinyanga Mjini mara baaada ya Mkutano wa hadhara.
Picha na Sanga Festo Jr.

No comments:

Post a Comment