Monday, October 12, 2015

MKUTANO WA CCM JIMBO LA CHONGA KUSINI PEMBA


5
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Chake chake Pemba Yussuf Ali Juma  Oktoba 11, 2015  wakati alipowasili katika uwanja wa mpira  Pujini Jimbo la Chonga Wilaya ya Chake chake Pemba wakati wa Mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu zinazoendelea.
6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi mara alipowasili  katika uwanja wa mpira  Pujini Jimbo la Chonga Wilaya ya Chake chake Pemba wakati wa Mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu zinazoendelea.

1
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokuwa akiwasalimia Wananchi na WanaCCM waliofurika katika uwanja wa mpira Pujini Jimbo la Chonga Wilaya ya Chake chake Pemba wakati wa Mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu zinazoendelea.
2
KIKUNDI cha Karafuu Band kutoka Dar es Salaam kikipiga muziki wake ili kuwaburudisha Wanachama cha Mapinduzi (CCM) na Wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi Mkuu zilizofanyika Oktoba 11, 2015 katika uwanja wa mpira Pujini Jimbo la Chonga Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba.
3
Maelfu ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM waliofurika katika mkutano wa hadhara wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo kijiji cha Pujini  Wilaya ya Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba katika Jimbo la Chonga wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa sera za CCM na kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuongoza tena katika kipindi cha pili cha Uongozi.
4   7
Baadhi ya WanaCCM na Wananchi wakisikiliza sera za Chama cha Mapinduzi (CCM) zilizotolewa na wajumbe mbali mbali wa katika mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi Mkuu zilizofanyika leokatika uwanja wa mpira kijiji cha Pujini Jimbo la Chonga Wilaya ya Chakechake mkoa wa Kusini Pemba,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.

No comments:

Post a Comment