Sunday, October 11, 2015

MGOMBEA UDIWANI MBAGALA RAIS WA YANGA AWEKA HISTORIA LEO YA MAFURIKOZ ONA HAPA



Mgombea Udiwani kupitia Kata ya Mbagala Kuu, Yusufu Manji akiongea na WANANCHI walioudhuria Mkutano wake wa kampeni uliofanyika leo Oktoba,11, 2015 viwaja vya Zakheem. Katika Mkutano huo Manji aliwaeleza wapiga kura wake kuwa kwa kushirikiana na familia yake watahakikisha wanaboresha Shule zilizoko Kata ya Mbagala Kuu ili ziweze kutoa Elimu Bora itakayozifanya ziwe za mfano  katika Kanda Afrika  Mashariki







Mfanya Biashara Maarufu, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na Mgombea Udiwani Kata ya Mbagala KUU-CCM akiongea na wakazi wa Mbagala katika viwanja vya Zakheem




Mgombea Ubunge Jimbo la Ilala Bwana Azzan Zungu-CCM akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mgombea wa  Udiwani wa Kata ya Mbagala Kuu Yusufu Manji viwanja vya Zakheem ambapo katika mkutano huo Zungu alisababisha kutokea kwa Vurugu  zilizofanywa na waliodaiwa kuwa wafuasi wa vyama vya Upinzani baada ya kuifananisha  ishara yao ya kuzungusha Mikono na Kipindupindu


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbagala Mangungu Issa (aliyenyoosha mkono) akimtambulisha Mwenyekiti wa Uvccm Taifa, Bwana Sadifa


Sadifa akimwaga sera

Manji akisisitiza jambo


Yusufu Manji akizungumza na mamia ya wakazi wa Mbagala katika viwanja vya Zakheem


No comments:

Post a Comment