2. Mkapa alipounda baraza jipya la mawaziri mwaka 1995 alikuacha, wengi wanasema kuwa Nyerere alimuambia asikupe hata uwaziri, Je kwanini Mwalimu alikukataa?
3. Tangu mwaka 1994, zaidi ya miaka ishirini sasa (20 years), Afrika kusini imekuwa ikikodisha nyumba yako masaki kama ubalozi wake, kuna tetesi kwamba huko nyuma walitaka kuhama lakini wakaogopa kuihama nyumba inayomilikiwa na kiongozi mkuu, na kulikuwa na tetesi kwamba wanataka kuhama lakini wanatishiwa. Ni kiasi gani cha fedha umepata kwa zaidi ya miaka 20 ya kukodisha nyumba hiyo? Je kiasi hicho kimeripotiwa kwenye fomu ya maadili?
4. Kuna maelezo kwamba nyumba hiyo ya ,masaki ambayo mzee mandela alikuja mwaka 1994 kuufungua ubalozi mpya wa afrika kusini ndicho chanzo kikuu cha mwalimu kusema inakuwaje kijana wa miaka 41, akiwa mtumishi wa umma maisha yake yote na mshahara wake unajulikana, anamiliki hekalu kama lile na tena kukodishwa na serikali ya kigeni? unasemaje kuhusu hili?
5. Pia unamiliki ranchi kubwa sana kule mzeri handeni, ranchi hiyo ilikuwa ranchi ya taifa, lakini ukajimegea na ukamega maeneo mengi zaidi. Ranchi iyo uliipata ukiwa bado kiongozi wa Umma, Je, mtu aliyewahi kuwa waziri wa mifugo na waziri mkuu, kujiuzia ranchi iliyokuwa ya serikali, inaendana na dhana ya uongozi uliotukuka??? Tukikupa madaraka makubwa zaidi, hautajiuzia kila kitu?
Vilevile, katika nchi ambayo wananchi wengi hawamiliki ardhi, Je, kiongozi kuhodhi eneo kubwa la ardhi, inatupa picha gani wananchi?

6. Kwenye sakata la Richmond, ujasiri nikusema ukweli au kubwaga manyanga? Kama ungesema ukweli na usingejiuzulu kwenye richmond, chama kingeathirika vipi wakati unasema hakuna kosa lililoanyika?
7. Kwanini kwenye kila tukio la kitaifa, ukisimama tu karibu na kikwete, unahangaika kutuma picha kwenye magazeti na mitandao yote?
8. Katika miaka yako 40 ya utumishi wa Umma, una lipi jipya ambalo umelisahau, na sasa utalifanya katika huu urais wako unaougharamia kwa pesa nyingi?
9. Umekuwa waziri wa ardhi, mbona matatizo bado tele nchini? Umekuwa waziri wa maji, mbona matatizo bado tele nchini? Umekuwa waziri wa mazingira, mbona kuna matatizo ya uharibifu na uchafuzi wa mazingira? Umekuwa waziri wa mifugo, mbona wafugaji bado masikini, na wanahangaika? Huo urais unautaka wa nini kama uwaziri umekushinda?
10. Umetoa mchango gani kwenye bunge maalum la katiba katika kuyatetea maoni ya wananchi, hali ulikuwa ukishuhudia yakipotoshwa na chama chako?
(itaendelea)