Friday, October 23, 2015
ZUHURA YUNUS UZURI WA SURA YAKE UNATAFSIRI AINA YA AKILI ALIYONAYO.
Kama umebahatika kusikiliza mahojiano yaliyofanyiwa na mtangazaji wa BBC Zuhura YUNUS na Mgombea uraisi wa ukawa Edward Lowassa utakubaliana na Mimi kuwa Mungu alimpendelea Zuhura alimpa akili kubwa na sura nzuri.
Lowassa kwa mara ya kwanza alikutana na mwandishi wa habari. Mwandishi mwenye weledi mkubwa, mwandishi usiyekuwa na njaa.
Zuhura ni mwandishi aliyemfanya Lowasa kukubali kwamba ana Ngombe nyingi huko vijijini na kwa mara ya kwanza Lowasa anakubalika kuwa atakwenda kuchunga Ngombe wake baada ya kustaafishwa siasa.
Zuhura ndiye mtu pekee Lowasa anayeona kuwa kwa ukubwa wa akili yake kuendelea kumhoji ni kumuonea. Kwa kaliba ya Lowasa, pesa zake, na kabila analotokea na kukulia kukubali kusema kuwa anaonewa tena na mwanamke si jambo la kitoto.
Zuhura ndiye mwandishi pekee ambaye anamfanya Lowasa aseme elimu bure ataitoaje. Mara nyingi Alikuwa hataki kusema source ya fedha za kuwasomesha watanzania bure atazitoa wapi. Ila probing ya Yunisi inatuwezesha watanzania kufahamu anategemea gesi ambayo faida yake tutaanza kuipaipata miaka sita ijayo. Anatufanya wengine tufahamu kwamba mpaka sasa Lowasa hajui garama za watanzania wote kusoma bure ndio maana anatasema pesa za mashangingi zitatosha.
Aidha Zuhura YUNUS kamfanya Lowassa akubali kwamba yeye ni fisadi. Unaweza kushangaa kakubalije. Kimazingira ni kwamba Lowassa tayari kashakubali kuwa ni fisadi. Kila swali alilowahi kuulizwa kuhusu ufisadi kama hakuliahirisha kutoa jibu basi alijikanganya nitatoa mfano.
Kwa mara ya kwanza alipoatangaza nia yake na ndoto yake kwa waandishi wa habari nyumbani kwake DODOMA aliulizwa kuhusu Richmond akasema atalitolea ufafanuzi Arusha kwenye kutangaza nia ila siku yenyewe alipofika hakuzungumzia chochote.
Alipokuwa anajiuzulu uwaziri Mkuu Bungeni alisema tatizo ni uwaziri Mkuu ila yeye si fisadi wala hausiki na Richmond.
Alipochukua form akiwa Ukawa jijini Daresalam Lowasa anasema kuwa Richmond hausiki nayo ila alipokea maagizo kutoka juu.
Alitaka tena kumpigia chenga Zuhura YUNUS ila kakutana na kichwa kaishia kusema kuwa swala la UFISADI linahitaji mjadala mpana na kuanza kulia lia kuwa anaonewa.
Lowasa kashindwa kutumia majukwaa na fursa zote hizo kutuezea na kututoa Shaka kuhusu kuhusika kwake na Richmond kwa nn wanatukimbia? Kwa nini anakuwa muongo? Kwa nini tusiamini kuwa Lowassa ni fisadi? .
Zuhura katusaidia sana kumfahamu huyu mtu. Hongera Zuhura YUNUS hongereni BBC.
Thadei Ole Mushi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment