Thursday, October 8, 2015

MREMA AWATAKA WAKAZI WA VUNJO KUMPIGIA KURA MAGUFULI



 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Ndugu Augustino Lyatonga Mrema mara baada ya kukutana njia panda ya Himo.
 Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Ndugu Augustino Lyatonga Mrema akizungumza mbele ya mgombea wa urais kupitia CCM na kuwataka wananchi wa Vunjo kumpigia kura mgombea wa urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwani ni rafiki wa kweli kwa maendeleo ya Tanzania.
 Wakazi wa Rombo Tarakea wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge jimbo la Vunjo kupitia CCM Innocent Shirima.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mwanga kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaahidi wananchi hao kuwa atatua tatizo la maji na barabara.
 Wananchi wa Mwanga mkoani Kilimanjaro wakifuatilia kwa makini mkutano wa kampeni za CCM
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mwanga ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa amejiandaa kutumikia wananchi kwa maendeleo ya Taifa.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Mwanga Profesa Jumanne Maghembe kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika Mwanga.

 Mhe. Christopher Ole Sendeka akiwasili kwenye uwanja wa mikutano Ndugu , Same Mashariki.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli pamoja na mgombea ubunge wa jimbo la Same Mashariki Mama Anne Kilango wakiwasalimu wakazi wa Same waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni za CCM Ndungu.
 Wakazi wa Same Mashariki wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Same Magharibi kwenye uwanja wa Kwasakwasa ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa katika uongozi wake atahakikisha kodi ndogo ndogo zinaondolewa kwa wafanyabiashara wadogo.

No comments:

Post a Comment