Thursday, October 8, 2015

MOSHI MJINI WASEMA BAI BAI KWA LOWASSA NA CHADEMA


Mh. Magufuli  Akimnadi Mgombea ubunge wa Moshi Mjini Mh. Davis Elisa Mosha.




Mkutano wa Kampezi za  Mgombea Urais Kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro umeendelea leo kwa kufanyika katika Jimbo la Moshi mjini. Mkutano huo uliofanyika leo Alaasiri katika Viwanja vya Mashujaa ulihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa CCM wa Wilaya, Mkoa na Kitaifa.

Wagombea na viongozi mbalimbali wakiimba wimbo maalumu wa Amani na Umoja.

Mbali na Mgombea Urais kupitia Tiketi ya CCM ndugu John Pombe Magufuli alikuwepo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya ccm na Mlezi wa Mkoa wa Kilimanjaro Ndhugu Emanuel Nchimbi. Pia kati ya watu walioongoza Msafara huo ni Pamoja na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Simanjiro Mh. Ole Sendeka.
Akizungumza na Wakazi wa Moshi Mjini Mh. Ole Sendeka aliwasihi wanachama wa CCM na wapenzi wa CCM kuepukana na Kuwajibu wanachama na Wafuasi wa Vyama vinavyounda ukawa kwasababu Ukawa wamedhamiria kuchokoza wana ccm ili kutokee MAchafuko ambayo Nchi za Magharibi zitaona ni CCM ndio wameleta vurugu.

Mh. John Magufuli akizungumza na Halaiki ya watu mjini Moshi.

Akizungumza na wakazi wa Moshi Leo Mgombea Urais Mh. John Pombe Magufuli aliweza kumzungumzia Mh. Davis Mosha ambaye ni Mgombea ubunge Kupitia Tiketi ya CCM ndani ya Jimbo la Moshi mjini. Magufuli alisema Hana shaka na Davis Mosha kwa kuwa anaelewa ni Mchapakazi na Mtekelezaji. Amekua mmoja wa Vijana wa kitanzania wenye mafanikio Makubwa kwa kuwekeza vyema katika nchi yetu ya Tanzania. Mh. Magufuli alimuahidi Ndugu Mosha kilometa kumi ya lami ndani ya Jimbo la Moshi mjini iwapo tu wana Moshi watamchagua. 


“Davis Aliniambia kuwa Moshi inamaeneo Mengi Muhimu ambayo Barabara zake sio kiwango cha Lami, Na mimi namuahidi Nitamletea Kilometa kumi za Barabara ndani ya Moshi Mjini”
Alisema Mh. Magufuli huku Akishangiliwa na Umati mkubwa wa watu.

Halaiki ya watu katika mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais na Ubunge wa ccm


Hata hivyo Mh. Davis Mosha aliwaasa wananchi wa Moshi Mjini wasifanye makosa na kuwaambia huu ni wakati wa maendeleo na Moshi Mjini itajengwa na watu wa Moshi hivyo wampatie Kura za Urais kwa Dr. John Pombe MAgufuli na Kura za Ubunge kwa Davis Mosha huku Madiwani wapewe wa Chama cha Mapinduzi ili kuweza kufanya kazi kwa Pamoja ya Maendeleo ya Moshi Mjini. 




Mh. Davis Mosha Mwenye shati la njano wapili kulia akiongoza Madiwani wake katika zoezi la Nguvu na Afya.
Mh. Davis Mosha akiwa na Wakereketwa wa ccm Moshi Mjini

No comments:

Post a Comment