Saturday, October 10, 2015
MGOMBEA UBUNGE CHADEMA AHUKUMIWA KIFUNGO MIEZI 6
Mgombea ubunge katika Jimbo la Kilombero mkoani Morogoro kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Peter Lijuakali amehukumiwa kifungo cha nje cha miezi sita baada ya kukutwa na hatia ya kumtukana ofisa
mtendaji wa kata. Mahakama wilayani Kilombero imetoa hukumu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi ambao umethibitisha kuwa mgombea huyo alimtukana ofisa mtendaji wa kata ya Ifakara, Afuley Mwenga.
Hata hivyo, Oktoba 12, mwaka huu, mahakama hiyo itaamua juu ya tuhuma nyingine inayomkabili Lijuakali ya kutishia kumuua mtendaji huyo wa Ifakara. Wafuasi wa Chadema waliokusanyika mahakamani hapo walionyesha nyuso za furaha kwani walidhani mahakama hiyo ya wilaya ingemhukumu mgombea wao kwenda jela.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment