Monday, October 12, 2015

MAMA SAMIA AFUNIKA JIMBO LA GEITA MJINI LEO

 Maelfu ya wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipohutubia mkutano wa kampeni leo katika jimbo la Geita mjini mkoani Geita leo
 
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni aliofanya leo katika jimbo la Geita mjini mkoani Geita leo
 William Mabula aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la geita mjini kwa tiketi ya Chadema, lakini chama hichi kikamuengua dakika za mwisho baada ya kushinda kura za maoni kisha kupachikwa mwingine aliyehamia chama hicho kutoka CCM, akitangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika jimbo hiko mkoani Geita leo
 Mkuu wa mkoa wa Geita, akimtuza, William Mabula aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la geita mjini kwa tiketi ya Chadema, lakini chama hichi kikamuengua dakika za mwisho baada ya kushinda kura za maoni kisha kupachikwa mwingine aliyehamia chama hicho kutoka CCM, wakati akitangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika jimbo hiko mkoani Geita leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan akimpongeza William Mabula aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la Geita mjini kwa tiketi ya Chadema, lakini chama hichi kikamuengua dakika za mwisho baada ya kushinda kura za maoni kisha kupachikwa mwingine aliyehamia chama hicho kutoka CCM, baada ya kutangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hiko mkoani Geita leo
Baadhi ya wanachama waliokuwa wa Chadema wakisubiri kuhamia CCM, kumfuata William Mabula aliyekuwa Mgombea Ubunge jimbo la geita mjini kwa tiketi ya Chadema, lakini chama hichi kikamuengua dakika za mwisho baada ya kushinda kura za maoni kisha kupachikwa mwingine aliyehamia chama hicho kutoka CCM, baada ya kutangaza kuhamia CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika jimbo hiko mkoani Geita leo. jumla ya vijana 61, walijiunga CCM
 Mgombea Ubunge jimbo la Geita mjini, Costantine Kanyasu, akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni uliofanywa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, katika jimbo hilo mkoani Geita leo
 Mgombea Ubunge jimbo la Geita Vijijini Joseph Kasheku maarufu kwa jina la King Msukuma, akihutubia mkutano wa kampeni uliofanywa na Mama Samia katika jimbo la Geita Mjini mkoani Geita leo
Msanii wa Bongo Movie anayeko katika kundi la Nimestuka, akionyesha machejo yake katika mkutano wa kampeni uliofanywa leo katika jimbo la Geita mjini mkoani Geita leo 
 Vijana wanaounda kundi la kampeni la Nimestuka, wakishambulia jukwaa wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Geita mjini mkoani Geita 
 Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva anayeko katika kundi la Nimestuka, Juma Kiroboro maarufu kwa jina la Juma Nature, akishambulia jukwaa akiwa na Ispekta Haruna wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, uliofanyika leo katika jimbo la Geita mjini mkoani Geita
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akiwapongeza Juma nature na Inspekta Haruna baada ya kutumbuiza katika mkutano wa kampeni aliofanya katika jimbo la Geita mkoani Geita leo
 Kiongozi wa kundi la kampeni la Mama sema na Mwanao, Steve Nyerere akimuombea kura Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Geita mkoani Geita leo
Msanii wa Bongo Movie ambaye pia ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Snura Majanga, akitoa burudani wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika leo katika jimbo la Geita mjini mkoani Geita leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments:

Post a Comment