Saturday, October 3, 2015

Mafuriko ya Dr. Slaa HAYAKUVUNA KITU ndio aweze Lowassa

Katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu kumetokea hoja moja inayoonekana kuthaminiwa sana na Public, hoja ya kujaza Wananchi wengi kwenye Mikutano ya Kampeni, tujikumbushe kidogo hii ilikuwa ni Mikutano ya Dr. Slaa na Chadema Mwaka 2010 ndipo kwa mara ya kwanza kati ya Wapiga kura Millioni 20.4 waliojiandikisha ni Millioni 8.6 tu waliopiga kura na kati yao Dr. Slaa alipata Millioni 2.3 ukilinganisha na CCM waliopata Millioni 5.6, je inawezekana Lowassa na UKAWA wakapata kura Millioni 18 wanazodai kati ya wapiga kura Millioni 24 waliojiandikisha Mwaka huu? Maana yake itakuwa kwamba Lowassa atakuwa ameongeza kura Millioni 16 yaani 800% itakuwa ni Historia ya Dunia kwa Mgombea Urais wa kwanza Duniani kukataa Midahalo na Wagombea wengine na kushinda kwa kura hizo za ajabu sana.


No comments:

Post a Comment