1. Mabadiliko. Lakini mabadiliko maana yake nini?
2. Elimu bure? Sawa, tueleze kivipi?
3. Elimu bure, afya bure, kuondoa kodi ya mfanyakazi, kupunguza ushuru kwa wawekezaji na wafanyabiashara wadogo wadogo, kutotegemea misaada?
4. Hivi kweli? Fedha ya kutoa vitu bure itatoka wapi bila kodi?
5. Kwenye gesi? Lakini hadi leo gesi hata haijaanza kutoa hiyo faida. Tunaambiwa faida ni ndani ya miaka 6 ijayo angalao, je mpaka miaka 6 inaisha hivyo vitu bure vitakuwa vinatolewaje?
6. Kwa mkopo? Toka kwa nani? Tutalipaje huo mkopo?
UKAWA SERA ZENU NI ZIPI? MBONA HAZIELEWEKI? MBONA ZIMEKAA KIJANJA JANJA NA HAZIWEZEKANI?
No comments:
Post a Comment