Friday, October 16, 2015

Jenerali afungwa kwa kushindwa na Boko Haram

Boko HaramImage copyrightAFP
Image captionWanajeshi wa Nigeria wamekuwa wakipiga hatua katika kukabiliana na Boko Haram karibuni
Mahakama ya kijeshi nchini Nigeria imemhukumu kifungo cha miezi sita jela jenerali aliyeongoza wanajeshi walioshindwa vibaya na Boko Haram.
Jenerali Enitan Ransome-Kuti amepatikana na hatia ya kukosa kutekeleza majukumu yake wapiganaji hao wa Kiislamu waliposhambulia mji wa kaskazini mashariki wa Baga, Januari.
Raia wengi waliuawa baada ya Boko Haram kuteka mji huo. Wapiganaji hao pia walifanikiwa kuteka shehena kubwa ya silaha.

Wakili wa jenerali huyo amesema atakata rufaa.
Shtaka jingine la kuwa mwoga liliondolewa.
Idadi hasa ya watu waliouawa wakati wa shambulio hilo mjini Baga bado haijabainika serikali ikidai ni watu 150 waliofariki lakini wenyeji wanadai huenda idadi hiyo ikafika 2,000.
Kando na kuua watu wengi, Boko Haram waliwateka wanawake wengi ambao waliwatumia kama watumwa wa ngono.
Mahakama ya kijeshi mjini Abuja imesema Jenerali Ransome-Kuti alifanya vyema kuwaagiza wanajeshi wake wajiondoe uwanja wa mapigano baada ya kuzidiwa nguvu lakini wakasema alifaa kuitisha usaidizi na kushambulia tena kwa lengo la kuuteka mji huo tena.
http://www.bbc.com/swahili/habari/2015/10/151016_jenerali_boko_haram_kushindwa_afungwa

No comments:

Post a Comment